REKODI NI YA SUNDOWNS, SIO CHIEFS- MMODI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, May 2, 2024

REKODI NI YA SUNDOWNS, SIO CHIEFS- MMODI.


Na Carlos Claudio.

Winga wa Kaizer Chiefs, Pule Mmodi anasema hakuna shinikizo la ziada la hofu kuwakabili Mamelodi Sundowns ambayo haijapoteza kwenye Uwanja wake wa nyumbani wa FNB.


Kaizer Chiefs wataikabili Mamelodi Sundowns katika mchezo wa ligikuu nchini Afrika Kusini ya DSTV Premiership Alhamisi Mei 2 majira ya saa 1:30usiku (CAT) katika dimba la FNB.


Mmodi, 30, amekuwa na msimu mseto wa kucheza Amakhosi tangu kuhama kutoka Golden Arrows kama mchezaji huru.


Huku Chiefs wakiwa katika nafasi ya nane kuelekea mchezo huo, Sundowns wanaweza kunyakua taji lao la saba mfululizo la ligi kwa ushindi katika uwanja wao wa nyumbani.


"Tutafanya kila tuwezalo kuishinda Sundowns, rekodi (ya kutopoteza) ni kwao, sio kwetu. Mwisho wa siku tutafanya kila tuwezalo kushinda mchezo huo,” Mmodi alisema.


"Hautakuwa mchezo rahisi kwetu na kwao, kwa hivyo nadhani tutafanya kila tuwezalo kushinda mchezo."


Mmodi alikanusha uchezaji wa Sundowns wa kutopoteza katika mechi 47 bila ya kushindwa ukilinganisha na mpinzani mwingine yeyote kwenye ligi na akaendelea kupendekeza kuwa atajaribu kuongeza mabao yake manne na asisti tatu kwenye mashindano msimu huu.


“Ni hisia za kawaida kwangu, nimecheza mechi nyingi sana dhidi ya Sundowns, hakuna tofauti kubwa kati yao kwa jinsi wanavyocheza, wanapenda kushika mpira lakini nadhani kwa siku zinazofuata tutajiandaa vyema kwa ajili yao kuwapachangamoto,” aliongeza.


"Kwangu mimi, lazima nithamini kuwa kiongozi [mchangiaji wa mabao] katika timu, nikitarajia michezo hii ambayo tumebakiza (msimu huu), nitajaribu kufunga mabao zaidi," aliongeza.


"Kuichezea Kaizer Chiefs kunakuja na presha nyingi, ni timu kubwa, ikiwa umesajiliwa, unahitaji kujitolea kucheza hapa. Sio kosa kwangu kuwa hapa, waliniona, kocha Arthur Zwane aliniona na kuniomba niisaidie timu kusonga mbele.”




No comments:

Post a Comment