Jumuiya ya Maendeleo ya nchini za Kusini mwa Afrika (SADC), imetangaza kuwa vikosi vyake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo vitafanya mashambulizi, kwa ushirikiano na vikosi vya serikali, ili "kuwamaliza waasi wa M23 na kurejesha amani na usalama."
SADC ilitangaza hayo katika taarifa yake ikilaani shambulio la bomu dhidi ya kambi ya wakimbizi wa ya Mugunga nje kidogo ya mji wa Goma, ambalo inasema lilitekelezwa na M23, kusababisha vifo vya watu takriban watu 16 na kujeruhi wengine takriban 30.
M23 walikanusha vikali madai hayo. Gavana wa Jimbo la Kivu, Ruguru, alisema kuwa watu 14 walifariki na wengine zaidi ya 35 kujeruhiwa katika shambulio la kambi ya Mugunga.
Vikosi vya SADC vimekuwa Kivu Kaskazini tangu mwishoni mwa mwaka jana, tangu Januari (1) vimeshiriki katika makabiliano ya "moja kw amoja" dhidi ya M23 kwa kutumia "mizinga nzito, ndege za kivita, ndege zisizo na rubani, na vifaru" katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa M23, kama mkuu wa M23 alivyotangaza wakati huo.
Maswali yamekuwa yakiulizwa ikiwa onyo hili jipya kutoka kwa vikosi vya SADC linamaanisha kwamba vikosi hivi, hasa kutoka Afrika Kusini, vitatumia nguvu za kijeshi za ajabu katika mzozo huo.
Mwezi uliopita, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akiwa nchini Rwanda, aliwaambia waandishi wa habari kwamba ana "nguvu mpya na azma" ya kutafuta "suluhisho la kisiasa" la mzozo wa DR Congo.
Taarifa ya SADC iliyotolewa siku ya Jumapili ilisema kwamba vikosi vyake lazima vifanye mashambulizi haya ili "kuwalinda raia na mali zao, wanaokabiliwa na tishio la kushambuliwa", "kufungua barabara ili kukidhi mahitaji", "na kulinda raia wanaokimbia kuua."
Serikali za Marekani na DR Congo zilithibitisha kwamba shambulio hilo lilifanywa na waasi wa M23 kwa msaada wa Rwanda. SADC pia ilithibitisha kwamba ilifanywa na M23.
M23 inakanusha kmadai hayo, ikilaumu vikosi vya serikali na waasi wa watiifu kwa serikali ya Kinshasa, ikisema kuwa walitumia silaha nzito karibu na kambi za wakimbizi.
Kujibu madai hayo, serikali ya Rwanda iliikosoa Marekani kwa "kufikia uamuzi mara moja wa kuilaumu Rwanda bila uchunguzi wowote", ikisema kwamba uchunguzi wa kuaminika lazima kwanza ukamilike ili kufichua kilichotokea.
Watu wengine 30 walijeruhiwa wakati makombora yalipopiga kambi za wakimbizi karibu na mji wa Goma mashariki mwa Kongo siku ya Ijumaa iliyopita.
Katika taarifa yake, serikali ya Rwanda iliikosoa Marekani kwa "kufikia uamuzi mara moja wa kuilaumu Rwanda bila uchunguzi wowote" ikisisitiza kwamba uchunguzi wa kuaminika lazima kwanza ukamilike ili kufichua ni nini hasa kilitokea.
kwa mjibu wa tangazo lilitolewa na msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo ,Rwanda haitabeba jukumu la shambulio hilo la makombora katika kambi za Mugunga na Lac Vert karibu na mji wa Goma , au kushindwa kwa utawala wa Congo kurejesha usalama mashariki mwa Congo.
Kwa upande mwingine ,tume ya umoja wa nchi za ulaya nchini DRC Katika taarifa yake haulaumu waasi wa M23 kwa mashambulizi haya dhidi ya wakimbizi, ingawa tume hiyo inashutumu kundi hilo kuendelea kusonga mbele_umeomba tu wahusika wafikishwe mbele ya sheria.
Ujumbe wa EU pia unalaani "kuongezeka kwa matumizi ya silaha nzito karibu na kambi za wakimbizi", ukisema kuwa "yana athari mbaya sana kwa idadi ya watu".
Katika taarifa yake, MONUSCO hailaumu upande wowote kwa mashambulizi haya kwa wakimbizi wa kambi ya Mugunga, lakini inazitaka pande zinazohusika na mzozo "kutunza maisha ya raia", na inaziomba mamlaka za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo "kuwafikisha mbele ya sheria" wahusika wa mashambulizi haya kwa sababu. "inaweza kuwa uhalifu wa kivita".
Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, alilaani mashambulizi hayo dhidi ya wakimbizi , na kuzihimiza pande zinazozozana kufikia suluhu la amani. Moussa Faki pia hakulaumu upande wowote kwa mashambulizi hayo.
Jeshi la Kongo na waasi wa M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda walilaumiana kwa mashambulizi hayo. Rwanda imekuwa ikikanusha kuunga mkono waasi wa M23 na kuishtumu serikali ya Congo kushirikiana na waasi wa Rwanda wa FDLR shutuma ambazo pia Congo inakanusha.
No comments:
Post a Comment