WIZARA YA UCHUKUZI YAOMBA BUNGE KUIDHINISHA BAJETI YA SH. TRILIONI 2.7 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, May 6, 2024

WIZARA YA UCHUKUZI YAOMBA BUNGE KUIDHINISHA BAJETI YA SH. TRILIONI 2.7


Na Okuly Julius , Dodoma

Katika mwaka wa fedha 2024/25 Wizara ya Uchukuzi imeomba kuidhinishiwa jumla ya shilingi trilioni 2,729,676,417,000 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo. 

Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema kati ya fedha hizo, Shilingi 114,744,476,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya kawaida na Shilingi 2,614,931,941,000 ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Waziri Mbarawa amesema haya leo Mei 6, 2024 jijini Dodoma, wakati akiwasilisha Bungeni mpango na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa Wizara hiyo katika mwaka wa fedha wa 2024/25



Prof.Mbarawa pia amegusia mafanikio yaliyopatikana ndani ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24 kuwa ni pamoja na uboreshaji wa kampuni ya ndege ya Tanzania (ATCL) ambao umeleta ufanisi wa utoaji huduma za usafri wa anga.

 Ambapo amesema hadi kufikia Machi mwaka huu ATCL imesafirisha abiria 850,660 ikilinganishwa na abiria 826,594 waliosafirishwa katika kipindi kama hicho kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 2.9.

"Maboresho haya yaliyofanywa na serikali imeiwezesha pia ATCL kusafirisha jumla ya tani 5,034 za mizigo ndani na nje ya nchi hadi kufikia mwezi Machi mwaka 2024 ikilinganishwa na tani 2,680.9 katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 87. 78, " ameeleza Prof. Mbarawa


Hivyo Prof.Mbarawa amesema katika mwaka wa fedha 2024/25, Serikali kupitia ATCL imeweka lengo la kukusanya jumla ya mapato ya Shilingi bilioni 717.97 kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani. Mapato hayo
yanatokana na huduma za kusafirisha abiria na mizigo ndani na nje ya nchi kwa kutumia
ndege zilizonunuliwa

Ameongeza kuwa Serikali kupitia
TCAA katika mwaka wa fedha 2024/25 itaendelea kutoa mafunzo katika kozi mbalimbali zinazohusiana na masuala ya usafiri wa anga kupitia Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC). Chuo hicho kinatarajia kudahili wanafunzi 2,500 na kuandaa kozi mpya nne (4).

Pia Prof. Mbarawa ameongeza kuwa katika mwaka wa
fedha 2024/25, Serikali kupitia TAA itaendelea kukisimamia Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro ambapo kupitia Kiwanja hicho jumla ya Shilingi bilioni 40.46 zitakusanywa
kutokana na huduma mbalimbali zitolewazo katika kiwanja hicho.


Kwa Upande wa Huduma za Bandari, Katika mwaka wa fedha 2024/25, Serikali kupitia Mamlaka
ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) itakusanya jumla ya Shilingi bilioni 1,837.78 kutoka katika vyanzo vya ndani vya mapato vitokanavyo na huduma za kibandari.

Katika hatua nyingine Prof.Mbarawa amegusia huduma za usafiri kwa njia ya reli ambapo amesema Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) inatarajia kukusanya Shilingi bilioni 118.89 kutoka katika vyanzo vyake vya
ndani kwa kusafirisha tani za mizigo 523,358, abiria 514,867 wa masafa marefu, abiria
2,315,551 wa masafa mafupi jijini Dar es Salaam kwa kutumia reli ya MGR na abiria 1,990,656 kwa kutumia reli ya SGR.

Ambapo amesema , Serikali katika mwaka wa fedha 2024/25 itaanza kutekeleza mkakati wa kuhakikisha SGR inaanza kufanya
kazi na kujiendesha kibiashara. Lengo la Serikali ni kutoendelea kutumia Ruzuku kuendesha reli ya SGR mara baada ya kukamilika. 


Ili kufikia azma hiyo, Serikali
itachukua hatua mbalimbali zikiwemo, kufungamanisha Reli zote Tatu za MGR, TAZARA na SGR kupitia Kidatu Transhipment ambapo reli zote hizo zitawasiliana kwa kuweka Gantry Crane
Storage Facilities pamoja na kuimarisha reli ya Morogoro, Kilosa hadi Kidatu kilometa 108.


Uunganishaji huu utawezesha usafirishaji wa mizigo kutoka Kusini mwa Afrika mpaka mikoa yote ya Tanzania pamoja na nchi Jirani pamoja na Kufungamanisha Bandari Kavu za Kwala, Isaka, Bandari za Mwanza na Kigoma na hatimaye Bandari za Dar es Salaam na Tanga kwa kuunganishwa na MGR na SGR. Njia hii pamoja na manufaa mengine itaongeza wigo wa matumizi ya Reli kwa mizigo ya ndani pamoja na inayotoka na
kuingia nchini.

No comments:

Post a Comment