KWAHERI DIRECTOR KHALFAN WASANII WATAKUKUMBUKA KWA VIDEO ZAKO. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, May 6, 2024

KWAHERI DIRECTOR KHALFAN WASANII WATAKUKUMBUKA KWA VIDEO ZAKO.


Aliyefahamika zaidi kama Director Khalfan, ila majina yake halisi ni khalfan Khamandro. Ni mmoja wa watayarishaji wa video nchini ambaye amefariki dunia Jumapili, Mei 5, 2024 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI), jijini Dar es Salaam.


Khalfan amezikwa jana saa 10 kwenye Makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam na ameacha mke ambaye ni mjamzito wa miezi saba na mtoto mwenye umri wa miaka mitano.


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano MOI, Patriki Mvungi alisema, "Ni kweli amefariki saa sita usiku wakati akiendelea na matibabu, Director Khalfani aliletwa hapa kwetu MOI akitokea Hospitali ya Taifa Muhimbili."


Hata hivyo, taarifa za awali zilieleza Khalmandro alifikishwa hospitalini hapo akiwa na tatizo la damu kuvilia kwenye ubongo, lililosababisha changamoto ya kupooza upande wa kulia wa mwili wake.


Enzi za uhai wake, Director Khalfan alijizolea umaarufu kutokana na kazi zake bora alizofanya na wasanii wakubwa kama Ben Pol, Christian Bella, Madee, Aslay, Shilole, Nu Mzinda, Maua Sama, Navykenzo, Baby Madaha, Chinbees, Bob Junior, Linah Sanga, Q Chilla, na wengine wengi.

No comments:

Post a Comment