TAMISEMI YATANGAZA MUHULA MPYA WA KIDATO CHA TANO 2024 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, May 30, 2024

TAMISEMI YATANGAZA MUHULA MPYA WA KIDATO CHA TANO 2024


Na Okuly Julius , Dodoma

Wanafunzi 188,787 waliokidhi vigezo wakiwemo wenye mahitaji maalumu 812 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano katika shule mbalimbali za Sekondari, pamoja na vyuo vya kati kwa mwaka 2024 hapa nchini.

Akizungumza leo Mei 30,2024 jijini Dodoma , Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI , Mohamed Mchengerwa amesema muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano utaanza Julai 1, 2024 ,hivyo wanafunzi wote waliochaguliwa wanapaswa kuanza kuripoti Shuleni kuanzia tarehe Juni


"Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia tumekamilisha zoezi la Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga na Kidato cha Tano katika Shule za Sekondari na Vyuo vya Elimu ya Ufundi vya Serikali kwa mwaka 2024 ambapo Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka Shule za Serikali, zisizo za Serikali na watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima,


Na kuongeza kuwa “Uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi umefanyika kwa kuzingatia ufaulu na nafasi zilizopo katika Shule; hivyo, hakutakuwa na fursa ya kufanya mabadiliko yoyote ya Shule kutokana na ukosefu wa nafasi”, amesema.

Pia , Mchengerwa ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa azma ya Serikali ya kuwa na Shule za Sekondari za Kidato cha Tano katika kila Tarafa inatekelezwa, ili kuwezesha wanafunzi wote wanaofaulu Mtihani wa Kidato cha Nne kupata nafasi ya kuendelea na masomo ya Kidato cha Tano na Sita.

“Upanuzi na ujenzi wa Shule Mpya za Kidato cha Tano na Sita uendelee kufanyika ikiwa ni pamoja na kuongeza tahasusi za masomo ya Sayansi, Mikoa ihakikishe inakuwa na tahasusi zote za msingi katika shule zake ili kuwapunguzia wazazi/walezi na wanafunzi gharama za usafiri kwenda shule za mbali”,amesema.

Watahiniwa 572,359 walifanya mtihani wa Kidato cha Nne kwa mwaka 2023, watahiniwa wa shule walikuwa 543,332 na wa Kujitegemea ni 29,027.

Amewapongeza walimu, wazazi na walezi wote kwa juhudi walizozifanya katika malezi na ufundishaji hali iliyowezesha wanafunzi kufaulu vizuri.

“Naomba wazazi/walezi wote tuendelee na moyo huu wa kusimamia na kufuatilia maendeleo ya watoto wetu ikiwemo kuwalea katika malezi na maadili mema ili wawe raia wema na wanaotegemewa na Taifa letu”, amesema.

Mchengerwa pia amewataka wanafunzi waliochanguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi kuendelea kufanya bidii katika kujifunza ili waweze kufanikiwa kujiunga na mafunzo ya elimu ya juu baada ya kuhitimu Kidato cha Sita na Vyuo vya Elimu ya Ufundi.

Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja, unaonesha kuwa watahiniwa 197,426 sawa na asilimia 37.42 walipata ufaulu wa Daraja la I – III, hali inayoonesha kuwa ufaulu wa watahiniwa wa mwaka 2023 umeongezeka kwa asilimia 0.47 ikilinganishwa na ufaulu wa Daraja la I – III wa watahiniwa 192,348 asilimia 36.95 wa mwaka 2022.

No comments:

Post a Comment