Afisa wa Habari na mawasiliano Azam FC Hashimu Ibwe amesema kuwa kama ikitokea timu hiyo itapelekwa kama wanavyopelekwa basi watachukua ligi Mara 10 mfululizo.
“Sisi nafasi ya pili tupo kwa mpira wetu , siku ikitokea tukapelekwa kama wanavyopelekwa wao nawaapia tunaenda kuwa mabingwa miaka 10 mfululizo na hamna wa kutuzuia.
“Wakiacha kudeka wajikaze kama sisi hawatoboi , tukianza kudeka kama wao na tukadekezwa tutakuwa mabingwa miaka 10 mfululizo.” amesema Ibwe.
Hayo yamekuja baada ya kikosi hicho kumaliza msimu wakiwa nafasi ya pili kwenye ligi msimu huu 2023/2024 uliyomalizika hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment