Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati wameshiriki maandamano ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani tarehe 01 Mei, 2024.
Maandamano hayo yalianzia katika viwanja vya Bunge na kuhitimishwa katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Maadhimisho hayo maarufu kama Mei Mosi kwa Mwaka 2024 yamebebwa na Kaulimbiu ya ”Nyongeza ya mishahara ni msingi wa mafao bora na kinga dhidi ya hali ngumu ya maisha”
No comments:
Post a Comment