WAZIRI BASHUNGWA AKUTANA NA BALOZI WA URUSI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, May 20, 2024

WAZIRI BASHUNGWA AKUTANA NA BALOZI WA URUSI.


Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Urusi nchini, Andrey Avetisyan katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Dar es salaam (JNICC), leo Mei 20, 2024.

Katika Kikao hicho wamejadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Urusi katika Sekta ya Ujenzi ikiwemo ufadhili wa elimu kwa vitendo kwa wanafunzi wanaomaliza masomo ya uhandisi katika vyuo vikuu hapa nchini. 

Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi na Wataalam kutoka Wizara ya Ujenzi na Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania wakiongozwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Aloyce Matei, Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Bernard Kavishe pamoja na timu ya watalaam kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS) ikiongozwa na Mtendaji Mkuu Mhandisi Mohamed Besta.

No comments:

Post a Comment