Na Okuly Julius, Dodoma
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji , ameliomba Bunge kuidhinisha
jumla ya shilingi bilioni 110.89 kwa Fungu 44 zitakazotumika na wizara hiyo ,katika mwaka wa fedha wa 2024/25
Ameyasema hayo leo Mei 21,2024 Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Makadirio ya Bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2024/25.
Ambapo amesema, kati ya fedha
hizo, shilingi Bilioni 81.11 ni matumizi ya kawaida, na shilingi Bilioni 29.78 ni matumizi ya Maendeleo. Kati ya shilingi Bilioni 81.11 za matumizi ya kawaida, zinajumuisha shilingi Bilioni
68.35 fedha za Mishahara na shilingi Bilioni 12.76 kwa ajili ya matumizi mengineyo.
VIPAUMBELE VYA BAJETI YA MWAKA 2024/2025
Katika mwaka 2024/2025,
vipaumbele vikuu vya Wizara ni sita (6). Aidha, vipaumbele
hivyo vitatekelezwa na shughuli mbalimbali za Wizara.
MOJA , Kuendelea na utekelezaji wa miradi ya kielelezo na
kimkakati;
MBILI , Kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji huduma
kwa kuimarisha miundombinu na mazingira wezeshi;
TATU ,Kuboresha mazingira ya uwekezaji viwandani na ufanyaji
biashara;
NNE , Kuchochea maendeleo ya watu kwa kuboresha miradi na
programu katika sekta za Kiuchumi na kijamii inayohusisha
elimu na mafunzo ya ujuzi;
TANO , Kufanya intelijensia ya masoko ya bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini kwenye masoko ya kimkakati na ya kimataifa; na
SITA , Kuchochea ukuaji wa Sekta binafsi nchini.
SHUGHULI ZITAKAZOTEKELEZWA KWA KUZINGATIA VIPAUMBELE VIKUU VYA WIZARA KATIKA MWAKA 2024/25
MOJA , Kuendeleza miradi ya kimkakati ya Magadi Soda Engaruka
na Makaa ya mawe Mchuchuma na Chuma cha Liganga;
MBILI , Kuendeleza miradi ya kiwanda cha viuadudu (TBPL) na
kiwanda cha KMTC;
TATU , Kuendelea kukiwezesha Kiwanda cha TBPL kuzalisha
mbolea hai (Biofertilizer) kwa kutumia mitambo iliyopo;
NNE , Kusanifu na kuendeleza utengenezaji wa vifaa tiba vya
hospitali awamu ya tatu;
TANO , Utengenezaji wa kibiashara wa viwanda vidogo vya
kuchakata sukari (sugar mill mini-processing plant -
Capacity 200 TCD);
SITA , Kutengeneza Mitambo ya nishati mbadala na teknolojia za wachimbaji wadogo wa madini (ASM) ili ziweze kusaidia katika utunzaji wa mazingira;
SABA , Kuanzisha mitaa ya viwanda kwa ajili ya kongano za
viwanda na biashara katika Wilaya moja kila Mkoa ili
kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi;
NANE , Kuendelea kupambana na uingizaji wa bidhaa bandia ili
kulinda nembo au alama za bidhaa dhidi ya watu
wanaotumia nembo/alama hizo bila idhini ya wamiliki;
TISA , Kufanya mafunzo kwa maafisa biashara kwa lengo la kuwafikia na kurahisisha shughuli za sajili na leseni kwa wafanyabiashara;
KUMI , Kuwarasimisha wafanyabiashara na wenye viwanda waliopo kwenye sekta isiyo rasmi kwa kuendesha kliniki za
biashara kwenye kila Halmashauri nchini.
KUMI NA MOJA , Kujenga uwezo na kutoa elimu kwa wadau kuhusu fursa zitokanazo na mashirikiano ya uwili, kikanda na kimataifa na kuwaunganisha wafanyabiashara wa Tanzania na
wawekezaji;
KUMI NA MBILI , Kuendelea na utafutaji wa masoko kwa bidhaa na huduma
zinazozalishwa nchini;
KUMI NA TATU , Kuingiza orodha ya bidhaa mpya kwenye mfumo na
kutanua mfumo ulioboreshwa kwenye maeneo ya mifugo,
uvuvi, madini yasiyo vito na bidhaa za mbogamboga;
KUMI NA NNE , Kukamilisha Mfumo wa Taarifa za Viwanda (National
Industrial Information Management System – NIIMS) na
tathmini ya viwanda na kuainisha fursa za uwekezaji
(Industrial Mapping) katika kanda ya Ziwa;
KUMI NA TANO , Kuimarisha usimamizi wa ubora na usalama wa bidhaa
nchini zikiwemo bidhaa za chakula na vipodozi;
KUMI NA SITA , Kukamilisha uandaaji wa kuzalisha Kinasaba cha Mafuta
(Fuel Marker) nchini; na
xvii.Kuimarisha uwajibikaji wa Wasimamizi wa Ghala kwa
kushirikiana na kampuni za uhakiki wa bidhaa katika ghala.
No comments:
Post a Comment