Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, amesema chama chake cha kisiasa - Umkhonto weSizwe (MK) - kitajiunga na muungano wa upinzani bungeni.
Alisema chama hicho kitajiandaa kutoa upinzani dhidi ya muungano unaoongozwa na African National Congress (ANC).
Pamoja na hayo, MK ilisema inashikilia kuwa uchaguzi wa mwezi uliopita uliibiwa na kutaka matokeo yafutiliwe mbali.
Hotuba ya Bw Zuma siku ya Jumapili ilisomwa na msemaji wa MK Nhlamulo Ndhlela ambaye alisema ANC haikuwa sehemu ya suluhisho tena.
Bw Zuma alisema hakuna serikali ya umoja wa kitaifa nchini Afrika Kusini na akaelezea ushirikiano huo kama "muungano usio mtakatifu unaoongozwa na wazungu kati ya DA na ANC ya Ramaphosa".
Chama cha ANC kilipoteza wingi wake wa kura kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa ubaguzi wa rangi na kuidhinisha makubaliano ya kugawana madaraka mwishoni mwa juma na chama cha Democratic Alliance (DA).
Vyama kadhaa vidogo pia vimejiunga na kile ANC inachokiita serikali ya umoja wa kitaifa. Wabunge wao Ijumaa walimchagua tena kiongozi wa ANC Cyril Ramaphosa kwa muhula wa pili kama rais.
No comments:
Post a Comment