RAISI WA TCCIA APONGEZA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA MATI SUPER BRANDS LIMITED - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, June 17, 2024

RAISI WA TCCIA APONGEZA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA MATI SUPER BRANDS LIMITED


Ferdinand Shayo ,Manyara.


raisi wa Chama cha Wafanyabiashara Tanzania (TCCIA) Vicent Minja ametembelea kiwanda cha kuzalisha vinywaji changamshi cha Mati Super Brands Limited na kujionea shughuli za uzalishaji zikiendelea ambapo amepongeza uwekezaji mkubwa ulioafanywa na Mwekezaji mzawa ambao umetoa fursa nyingi za ajira kwa vijana pamoja na kulipa kodi stahiki za serikali.


Minja amesema hayo katika ziara yake ya kikazi iliyofanyika mkoani Manyara ambapo amezungumza na Wafanyabiashara Pamoja na kutembelea kiwanda hicho chenye makao makuu Mkoani Manyara.



“Nawapongeza sana Mati Super Brands Limited kwa kufanya vizuri katika uzalishaji wa bidhaa bora na usambazaji wa bidhaa ndani ya nchi na nje ya mipaka ya nchi “ Anaeleza raisi wa TCCIA.

Mkurugenzi wa Kiwanda Cha Mati Super Brands Limited ameeleza kufurahishwa na ziara ya raisi wa TCCIA kwenye kiwanda hicho ambaye amefika na kujionea shughuli zinazofanywa na kiwanda hicho.


“Tunashukuru kupata ugeni wa raisi wa TCCIAKwetu sisi ni Faraja kuona viongozi wa wafanyabiashara wanatambua mchango wetu na kututembelea” Anaeleza Mkurugenzi wa Mati Super Brands Limited David Mulokozi.

No comments:

Post a Comment