DG MPYA TAEC ARIPOTI RASMI KAZINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, June 20, 2024

DG MPYA TAEC ARIPOTI RASMI KAZINI


 

Mkurugenzi Mkuu  wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania Prof. NAJAT KASSIM MOHAMMED ameripoti rasmi ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Jijini Dodoma leo na kupokelewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu ambaye pia ni Mkurugenzi wa kurugenzi ya Teknolojia ya Nyuklia na  huduma za ufundi Dkt. Remigius Kawala Pamoja na Mkurugenzi wa Huduma za Tume Bwn. Edgar Mbaganile sambamba na Menejimenti na wafanyakazi wa Tume.


Prof. NAJAT ameripoti ofisini Dodoma ikiwa ni siku chache tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN alipomteua kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAEC kuchukua nafasi ya Prof. Lazaro Busagala ambaye amemaliza muda wake.












No comments:

Post a Comment