|
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt.Dotto Biteko,akizungumza katika mkutano wa Teachers’ Breakfast Meeting uliowakutanisha walimu na maafisa elimu wa wilaya ya Dodoma Mjini wenye lengo la kuboresha ufaulu jiji la Dodoma ulioandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe.Anthony Mavunde,hafla iliyofanyika leo Juni 1,12024 jijini Dodoma. |
|
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akizungumza katika mkutano wa Teachers’ Breakfast Meeting uliowakutanisha walimu na maafisa elimu wa wilaya ya Dodoma Mjini wenye lengo la kuboresha ufaulu jiji la Dodoma ulioandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe.Anthony Mavunde,hafla iliyofanyika leo Juni 1,12024 jijini Dodoma. |
|
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde,akizungumza katika mkutano wa Teachers’ Breakfast Meeting uliowakutanisha walimu na maafisa elimu wa wilaya ya Dodoma Mjini wenye lengo la kuboresha ufaulu jiji la Dodoma ulioandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe.Anthony Mavunde,hafla iliyofanyika leo Juni 1,12024 jijini Dodoma. |
|
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akizungumza katika mkutano wa Teachers’ Breakfast Meeting uliowakutanisha walimu na maafisa elimu wa wilaya ya Dodoma Mjini wenye lengo la kuboresha ufaulu jiji la Dodoma ulioandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe.Anthony Mavunde,hafla iliyofanyika leo Juni 1,12024 jijini Dodoma. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri,akizungumza katika mkutano wa Teachers’ Breakfast Meeting uliowakutanisha walimu na maafisa elimu wa wilaya ya Dodoma Mjini wenye lengo la kuboresha ufaulu jiji la Dodoma ulioandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe.Anthony Mavunde,hafla iliyofanyika leo Juni 1,12024 jijini Dodoma. |
|
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt.Dotto Biteko (hayupo pichani) ,akizungumza katika mkutano wa Teachers’ Breakfast Meeting uliowakutanisha walimu na maafisa elimu wa wilaya ya Dodoma Mjini wenye lengo la kuboresha ufaulu jiji la Dodoma ulioandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe.Anthony Mavunde,hafla iliyofanyika leo Juni 1,12024 jijini Dodoma. |
|
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt.Dotto Biteko,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa Photocopiers 10 kubwa kwa lengo la kuchapisha mitihani na kuwapunguzia mzigo wazazi wa watoto wa Dodoma Jiji kuchangia fedha za mitihani ya majaribio ya kila wiki. |
|
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt.Dotto Biteko,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua mkutano wa Teachers’ Breakfast Meeting uliowakutanisha walimu na maafisa elimu wa wilaya ya Dodoma Mjini wenye lengo la kuboresha ufaulu jiji la Dodoma ulioandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe.Anthony Mavunde,hafla iliyofanyika leo Juni |
Na Mwandishi Wetu, DODOMA
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,Dk Doto Biteko amesema uamuzi wa Wizara ya Elimu kubadili vigezo vya kutangaza shule 10 bora zilizofanya vizuri katika mitihani ya taifa,jambo ambalo linasaidia kutokubagua wanafunzi.
Biteko alisema hayo leo Juni 1,2024, katika mkutano wa walimu wa halmashauri ya jiji la Dodoma.
Alisema walimu wanapaswa kutengeza Taifa kwa kuhakikisha wanazalisha kizazi ambacho kitakujakuwa na manufaa makubwa kwa nchi na kuwatenganisha.
"Hakikisheni mnazalisha wanafunzi waliobora msitumie kigezo cha akili kuwagawa wanafunzi mkifanya hivyo mtakuwa mnazalisha taifa lisilo Bora,"alisema DK Biteko.
Dk Biteko alisema mtu wa kwanza anaeweza kumtengeneza mtoto ni mwalimu hivyo wana wajibu wa kumtengeneza ili awe bora.
"Walimu mnayo kazi kubwa ya kututengenea Taifa kwa kutafsiri R4 za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan hasa kwenye suala la maridhiano,"alisema Dk Biteko
Mbali na hili,,amewataka walimu kujitahidi kuwafundisha kwa umakini ili wanafunzi wazidi kufanya vizuri na kutafsiri kwa vitendo maono ya Rais Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Anthony Mavunde katika kuhakikisha elimu bora inatolewa.
Dk Biteko alisema Mataifa yote yaliyoendelea uwekezanj wake upo katika elimu na ndiko alikowekeza Rais Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Mavunde alisema lengo la Mkutano huo ni kujadili changamoto katika sekta ya elimu katika muhula uliopita na wafanye nini katika muhula ujao ili kuendelea kuwatia moyo walimu.
"Tuliona Njia pekee ya kufanya vizuri ni kuwaweka walimu pamoja hatutaki mwalimu wetu akiwa na changamoto akalalamike kwani haya ni sehemu ya maisha yetu,"alisema Mavunde
Amesema kupitia Mkutano huo watazungumza kwa pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa kutatua kero ambazo zitajitokeza.
"Dhamira yangu ni ya dhati katika kukuza elimu kwani nimeweza kujenga shule za msingi na sekondari kwa wanafunzi waliokuwa wakitembea umbali mrefu,"amesema Waziri Mavunde.
Amesema kwa kushirikiana na baadhi ya wadau wameweza kujenga uzio katika shule mbalimbali ambao unasaidia watoto kusoma kwa utulivu.
Kwa upande wake Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof Adolf Mkenda amesema Mbunge wa Dodoma,Anthony Mavunde anathamini elimu na kila anapokutana nae huwa anahoji kuhusu miradi mbalimbali ya elimu katika Jimbo la Dodoma Mjini.
Dk Mkenda alisema kwenye miundombinu Rais Samia Suluhu Hassan wamejenga Vyuo vya Ufundi (Veta) 64 kwa mkupuo na Campus katika Vyuo Vikuu vyote katika maeneo mbalimbali.
"Tunapoenda kila Mkoa kutakuwa na Campus ya Chuo Kikuu lengo letu ni kuhakikisha elimu inakuwa karibu na wanafunzi,"amesema Prof Mkenda.
No comments:
Post a Comment