Na Okuly Julius Dodoma
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesmea ,katika utekelezaji wa
mpango na bajeti ya mwaka 2023/24, wizara hiyo
imekabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ,huduma hafifu ya matengenezo ya mashine za EFD.
Waziri Nchemba ameyasema hayo leo Juni 4 , 2024 Bungeni jijini Dodoma, wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Wizara ya Fedha kwa mwaka 2024/2025.
Pia Dkt.Nhemba amesmea , kukosekana kwa mtandao na mwamko mdogo wa
wananchi kudai na kutoa risiti za kielektroniki za
EFD pia ni chanzo cha kukwamisha utekelezaji wa Bajeti.
"kuongezeka kwa mahitaji ya ziada ya rasilimali fedha kutokana na athari za mabadiliko ya
tabianchi na baadhi ya walipakodi kuficha taarifa za miamala ya kibiashara na kuendelea kuwepo kwa
biashara za magendo, hususan mipakani na mwambao wa bahari ni chanzo cha kutotekelezwa kwa mpango na Bajeti", amesema
Dkt. Nchemba ameema , ili kukabiliana na
changamoto zilizojitokeza, wizara imechukua hatua
mbalimbali kama ifuatavyo:
i.Kuhamasisha matumizi ya mfumo wa Virtual Fiscal
Devices (VFD) kutoa risiti kama mbadala wa mashine
za EFD ,kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kudai na kutoa risiti za kielektroniki,kuimarisha soko la ndani la fedha ili kuwezesha
utekelezaji wa baadhi ya miradi kwa kutumia vyanzo
mbadala vya mapato,kufanya mapitio ya mipango na bajeti ili kugharamia mahitaji ya ziada ya kurejesha miundombinu iliyoathirika na mabadiliko ya tabianchi,
kuboresha mifumo ya usimamizi wa mapato
ikiwemo doria mipakani na mwambao wa bahari ili
kudhibiti biashara za magendo na udanganyifu; na na kufungamanisha mifumo ya mipango na bajeti
za kisekta na mifumo ya kukabiliana na mabadiliko ya
tabianchi.
No comments:
Post a Comment