FUNDI WA MITAMBO ADAI KUFUTWA KWA KUFICHUA HALI YA USALAMA WA BOEING. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, June 27, 2024

FUNDI WA MITAMBO ADAI KUFUTWA KWA KUFICHUA HALI YA USALAMA WA BOEING.

Richard Cuevas alidai kushuhudia utengenezaji wa chini ya kiwango kwenye sehemu muhimu ya ndege ya Boeing 787.


Fundi wa ndege ambaye alipewa kandarasi ya kukarabati ndege za Boeing amedai kuwa alibandikwa jina la "mnyang'anyi" na kisha kufutwa kazi kwa kutilia shaka hali ya usalama wa ndege za kampuni hiyo.


Richard Cuevas alidai kushuhudia utengenezaji wa chini ya kiwango kwenye sehemu muhimu ya ndege ya Boeing 787.


Boeing, ambayo imekuwa ikikabiliwa na maswali mengi kuhusu usalama wa ndege zake, ilisema masuala hayo yamechunguzwa na "hakuna dosari iliyopatikana."


Mawakili wanaomwakilisha Bw Cuevas walidai aliripoti masuala muhimu ambayo yanaweza kusababisha hatari kubwa ya usalama wa umma na amewasilisha malalamiko kwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga na Utawala wa Afya na Usalama Kazini.


Bw Cuevas, ambaye amefanya kazi katika tasnia ya usafiri wa anga kwa miaka 40, alipewa kandarasi ya Spirit Aerosystems, ili kufanya kazi kwenye ndege ya Boeing 787 yenye shinikizo kubwa, kuba kwenye eneo la mbele ya ndege ambayo hutumika kama kizuizi.


"Alitambua utendaji wa chini ya kiwango na kuelezea wasiwasi wake," mawakili wa Bw Cuevas walisema.


"Lakini Spirit na Boeing walishindwa kusimamisha mchakato mbaya wa utengenezaji." Kulingana na nyaraka za sheria, mfanyakazi mwenzake alisema: "Tuna mjanja kati yetu."


Bw Cuevas alisema alifutwa kazi na shirika la Aerosystems la Spirit mnamo Machi 2024.


Boeing aliiambia BBC: "Mfanyakazi wa mkandarasi mdogo hapo awali aliripoti wasiwasi kwetu ambao tulichunguza kwa kina, kwani tunachukua kwa uzito suala lolote linalohusiana na usalama."


Hata hivyo, masuala yaliyoibuliwa yalionekana kutowasilisha hofu ya usalama wa ndege na kwamba yalikuwa yameshughulikiwa, Boeing ilisema.


Msemaji wa Spirit Aerosystems Joe Buccino, alisema kampuni hiyo "inachunguza suala hilo".

No comments:

Post a Comment