![]() |
Mkazi wa Karachi akijaribu kutuliza joto mwilini |
Halijoto ilipoongezeka kusini mwa Pakistan, ndivyo miili ya waliofariki ilivyoongezeka.
Kampuni inayotoa huduma ya ambulensi ya Edhi inasema kwa kawaida huwapeleka takribani miili 30 hadi 40 katika chumba cha kuhifadhi maiti cha jiji la Karachi kila siku.
Lakini katika muda wa siku sita zilizopita, imekusanya miili 568 - 141 siku ya Jumanne pekee.
Ni mapema mno kusema ni nini hasa kilisababisha kila moja ya vifo hivyo.
Hata hivyo, kuongezeka kwa idadi ya waliofariki inakuja wakati halijoto mjini Karachi ilipopanda zaidi ya nyusi joto 40 (104F), huku unyevunyevu wa hali ya ukiifanya kuhisi joto kama 49C, ripoti zilisema.
Watu wamekuwa wakielekea hospitali kutafuta msaada. Hospitali ya umma ya Karachi iliwalaza watu 267 kutokana na mshtuko wa joto kati ya Jumapili na Jumatano, alisema Dk Imran Sarwar Sheikh, mkuu wa idara ya dharura
Kumi na wawili kati yao walifariki.
"Watu wengi tuliowaona wakiifika hospitalini walikuwa na umri wa miaka 60 au 70, ingawa kulikuwa na watu wapatao 45 na hata wanandoa waliokuwa na umri wa miaka 20," Dk Sheikh aliambia BBC.
Dalili walizokuwa nazo ni pamoja na kutapika, kuhara na homa kali, "Wengi wa wale tuliowaona walikuwa wakifanya kazi nje.
Tumewaarifu wahakikishe wanakunywa maji mengi na kuvaa nguo nyepesi kwenye joto hili la juu.
” Halijoto ya juu - inayoelezewa kama "wimbi la joto" na mtaalamu mmoja wa hali ya hewa - ilianza wikendi.
Vituo vya joto na kambi zilianzishwa ili kujaribu kutoa misaada kwa umma.
Picha zinaonyesha watoto wakicheza kwenye chemchemi walipokuwa wakijaribu kujituliza.
"Niangalie! Nguo zangu zimelowa jasho kabisa,” Mohammad Imran aliambia shirika la habari la Reuters alipokuwa akijitahidi kutuliza joto mwilini siku ya Jumatatu.
Sio wote waliohitaji msaada walifika hospitalini. Wasim Ahmed alibaini kuwa hajisikii vizuri alipofika nyumbani.
No comments:
Post a Comment