Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji (Rufaa), Jacobs Mwambegele akikabidhi nakala ya orodha ya vituo vyote vya kuandikisha wapiga kura kwa viongozi na wawakilishi wa Vyama 19 vyenye usajili kamili wakati Vyama hivyo vilipokutana katika mkutano wa Tume na viongozi wa vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 07 Juni, 2024 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari.
Mapema wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, Jaji Mwambegele aliahidi kuvipatia nakala hiyo vyama vyote na pia Vyama hivyo vitapatiwa nakala tepe ya orodha hiyo.
“Leo kila chama kitapewa nakala ya orodha ya vituo vyote vya kuandikisha wapiga kura. Dhumuni la kuwapatia nakala hizo ni kuwawezesha Kupanga na kuweka mawakala wa uandikishaji katika vituo vya kuandikisha wapiga kura,” amesema Jaji Mwambegele.
Vyama hivyo vilivyopokea ni AAFP, ACT - WAZALENDO, ADA - TADEA, ADC, CCK, CCM, CHADEMA, CHAUMA, CUF, Demokrasia Makaini, DP, NCCRA- MAGEUZI, NLD, NRA, SAU, TLP, UDP, UMD na UPDP.
No comments:
Post a Comment