Mbunge mteule wa Jimbo la Kwahani Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharib, Zanzibar, Bw.Khamis Yussuf Mussa akinyanyua juu hati yake ya ushindi baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi.
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kupitia Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani-Zanzibar Bi.Safia Iddi Muhammad imemtangaza Bw.Khamis Yussuf Mussa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mshindi wa Kiti cha Ubunge katika Jimbo la Kwahani.
Mbunge mteule wa Jimbo la Kwahani Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharib, Zanzibar, Bw.Khamis Yussuf Mussa akionesha hati yake ya ushindi baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani, Zanzibar Bi.Safia Iddi Muhammad akimkabidhi hati ya ushindi Bw.Khamis Yussuf Mussa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kumtangaza kuwa ndiye mshindi wa Kiti cha Ubunge katika Jimbo la Kwahani.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani, Zanzibar Bi.Safia Iddi Muhammad akisoma matokeo ya Jimbo la Kwahani.
Wagombea na mawakala wao wakifuatilia matokeo hayo.
Aliyekuwa Mgombea wa CCM, Bw.Khamis Yussuf Mussa 'Pele' akifuatilia kwa makini utangazaji wa matokeo. Wagombea na mawakala wao wakifuatilia matokeo hayo.
Wananchi wakisubiri matokeo.
Waangalizi wa Uchaguzi wa Kwahani wakisikiliza matokeo.
*************
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kupitia Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani-Zanzibar Bi.Safia Iddi Muhammad imemtangaza Bw.Khamis Yussuf Mussa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mshindi wa Kiti cha Ubunge katika Jimbo la Kwahani.
Jimbo la Kwahani lilikuwa na wapiga kura 11,936 na waliojitokeza kupiga kura ni 7,522 ambapo kura 139 zilikataliwa hivyo kufanya kura halali zilizopigwa kuwa ni 7,383.
No comments:
Post a Comment