Wakenya wanaandamana kupinga muswada mpya wa fedha unaotoa mapendekezo ya ushuru ambayo hayakupendwa na watu wengi ambayo yameibua hasira kote nchini.
Muswada huo tata, ambao una vifungu vinavyoonekana kuwatwisha mzigo mkubwa raia wa kawaida na wafanyabiashara, umezua kilio kikubwa kutoka kwa wananchi ambao tayari wameelemewa na gharama ya juu ya maisha.
Yameibua maandamano yanayoongozwa na vijana, ambayo, ingawa kwa kiasi kikubwa yamekuwa ya amani, yamesababisha takriban kifo kimoja na mamia ya majeruhi pamoja na kukamatwa kwa mamia ya watu - ambayo yote yamelaaniwa na wanasheria na makundi ya haki za binadamu.
Serikali imetupilia mbali baadhi ya mapendekezo yenye utata, lakini imechukua hatua chache kupunguza hasira za umma.
Wengi sasa wanataka muswada wote uondolewe inagwaje tayari wabunge wameshpitisha baadhi ya marekebisho yaliyopendekezwa na seriukali ili kutuliza hasira za umma .
Katika mitandao ya kijamii, kumekuwa na wito wa maandamano na madai kwamba wabunge wapinge nyongeza hiyo ya ushuru.
No comments:
Post a Comment