OR – TAMISEMI
Mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Arusha zimeanza vizuri mashindano ya UMITASHUMTA 2024 yaliyozana rasmi Juni 06, 2024 Mjini Tabora, baada ya kuibuka na ushindi mnono katika michezo iliyochezwa kwenye viwanja vya shule ya sekondari Tabora wasichana Asubuhi ya Juni 07, 2024.
Katika mchezo wa kwanza wa kundi A, ambao umechezwa kwenye uwanja A wa shule ya Sekondari tabora wasichana, Timu ya Mkoa wa Mwanza ilipata ushindi wa magoli 57 -06 dhidi ya mkoa wa Kagera, na mchezo mwingine wa kundi B ulishuhudia mkoa wa Geita ulipata ushindi wa magoli 58-01 kutoka kwa Iringa.
Mchezo mwingine ulizihusisha Arusha iliyoifunga Ruvuma magoli 22-09, Shinyanga ikaibuka na ushindi wa 22-15 dhidi ya Simiyu, huku Pwani na Katavi zikitoshana nguvu kwa sare ya magoli 19-19 na wenyi Tabora wakaishinda morogoro 51-11.
Akizungumzia michezo ya mwaka huu, Mratibu wa Mchezo wa Netiboli kwenye mashindano ya UMITASHUMTA 2024 Stella Mwangomali, amesema kuna maboresho makubwa yamefanyika hususan kwenye eneo la miundombinu pamoja na sharia za uendeshaji hali ambayo imechangia ukuaji wa michezo hiyo.
Kwa upande wao makocha wa Timu za mikoa ya Arusha Mwalimu Tulu Idd Ramadhani, na mwenzake wa Shinyanga Dovinas Jangola, wameelezea maandalizi ya mikoa yao katika mashindano ya mwaka huu, wakisema kuwa kumeongezeka ushindani unaosababishwa na wchezaji kuandaliwa vizuri.
Mashindano ya UMITASHUMTA & UMISETA 2024 yanayoendelea mkoani Tabora yananaandaliwa na kusimamiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim majaliwa, anatarajiwa kuzindua rasmi mashindano hayo Juni 08, 2024 kwenye Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mkoani Tabora, na kauli Mbiu ya mwaka huu ni “Tunajivunia mafanikio katika sekta ya elimu, michezo na Sanaa, Hima Mtanzania shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024”
No comments:
Post a Comment