Prof. Abel Makubi, Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) leo amekutana na Menejimenti ya Hospitali siku moja baada ya kuripoti ofisini.
Prof. Makubi amekutana na menejimenti mara ya kwanza tangia ameingia Hospitali ya Benjamin Mkapa kwaajili ya kuwatambua viongozi wa menejimenti na kutoa mweleko wa Hospitali katika uongozi wake.
“Leo tumekutana leo ili tutambuane na nijue ninanguvu kubwa kiasi gani nitakayo saidiana nayo kufanya kazi na kuipeleka BMH kuwa Hospitali ya Kitaifa na ya kisasa katika huduma bora” amesema Prof. Makubi
Akiongea na Menejimenti amewataka kuwasimamia wanaowaongoza kuhakikisha wanafanyakazi kwa kujituma, weledi, maadili na nidhamu ya hali ya juu katika kuwahudumia wagonjwa.
“Nafahamu mnafanya kazi nzuri inayoleta matokeo chanya BMH lakini wapo baadhi ya wataalamu wachache hawafanyi vizuri kwa kuchelewa kazini na kuwahi kutoka ninawaonya leo hiyo tabia waambieni waache, lengo letu liwe moja tu kumuhudumia mgonjwa kwa viwango vizuri , bila kuchelewesha na kuongeza ubunifu katika kutatua kero huku kila mmoja akiwa na moyo wa kuithamini BMH kama nyumba yake (sense of ownership) , amesema Prof. Makubi
Aidha, amesisitiza kutatua kero zote zinazowakabili wagonjwa ili mgonjwa anapoingia Hospitali mpaka anapotoka asitoke na manung’uniko ambayo si ya lazima na yako chini ya uwezo wetu.
“Sitegemei kusikia malalamiko mengi kutoka kwa wagonjwa hasa yale yaliyo ndani ya uwezo wetu, kila mtu ajipange namna bora ya kuwahudumia wagonjwa kwa kasi na kuzingatia miongozo (SOPs) , amesema Prof. Makubi.
Aidha Prof. Makubi amewaomba wajumbe wote kumpa ushirikiano, umoja na kuwa na moyo kushaurina, kushirikishana na watunishi wote katika kutatua changamoto na kujishusha kwa Wagonjwa/ndugu na Watumishi wote hasa wa chini ambao tunapaswa kuwasilikiza na kuwasaidia .
No comments:
Post a Comment