Na Okuly Julius, Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo amesema, Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati umeongezeka ambapo mwaka 2023, miradi ya kimkakati na uwekezaji katika sekta mbalimbali ilizalisha
ajira 162,968 za moja kwa moja ikilinganishwa na ajira 101,353 zilizozalishwa mwaka
2022, sawa na ongezeko la asilimia 58.7.
Prof. Mkumbo ametoa kauli hiyo leo Juni 13,2024, wakati akiwasilisha bungeni , taarifa ya hali ya uchumi kwa mwaka 2023 na Mpango wa maendeleo wa Taifa wa mwaka 2024/2025.
Prof. Mkumbo amesema, kati ya ajira zilizozalishwa, ajira 156,661 zilikuwa za watanzania na ajira 6,307 za wageni mwaka 2023 ikilinganishwa na ajira 95,831 za watanzania na ajira 5,522 za wageni mwaka 2022.
"Kuongeza kwa ajira za Watanzania kulitokana na juhudi za Serikali kuongeza fursa za ajira kupitia urithishaji wa ujuzi na uhaulishaji wa teknolojia kwa kuhakikisha mikataba inayoingiwa inaweka vipengele vya ushiriki wa Watanzania 470,"ameeleza Prof. Mkumbo
Aidha, Mwaka 2023, makandarasi wa miradi ya kimkakati waliingia mikataba na Kampuni. 3,360 kwa ajili ya kandarasi 1,032, kazi za ushauri elekezi 104 na huduma 2,224 za chakula, ulinzi, usafiri, bima na bidhaa za ujenzi ikilinganishwa na kampuni 2,827 mwaka 2022,sawa na ongezeko la asilimia 18.9.
Aidha, idadi ya wakandarasi wa kitanzania waliosajiliwa
walikuwa ni 1,690 na wakandarasi walioingia ubia ni 64 wa kutoa huduma katika miradi ya
kimkakati.
Katika hatua nyingine Prof. Mkumbo, amesema hadi kufikia March 2024, deni la Serikali lilikuwa shilingi bilioni 91,708.3 (Tsh. trilioni 91.7) ikilinganishwa na shilingi bilioni 77,010.4 (Tsh. trilioni 77.) katika kipindi kama hicho mwaka 2023, sawa na ongezeko la asilimia 19.1.
Mkumbo amesema “deni la ndani lilikuwa shilingi bilioni 30,753.8 na deni la nje lilikuwa shilingi bilioni 60,954.5”
No comments:
Post a Comment