NAIBU Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri Elimu, Prof. Razack Lokina amefungua Kongamano la Mtandao wa ekolojia ya Kisiasa (POLLEN2024) linalohusisha watafiti mbalimbali wanaofanya tafiti zao katika maeneo ya ekolojia na kuhusianisha na mambo ya kisiasa na Uongozi.
Prof. Razack amesema Mkutano huo maarufu wa POLLEN 2024, unaratibiwa na Mtandao wa Ekolojia ya Kisiasa, unafanyika kuanzia leo tarehe 10 hadi 12 Juni 2024.
"Mkutano huu utafanyika kwa wakati mmoja katika maeneo matatu Tatu tofauti na mabara matatu tofauti na nchi Tatu tofauti ambazo ni : Peru katika Mji wa Lima, Bara la Amerika Kusini , Tanzania katika jiji la Dodoma, Bara la Afrika na Sweden katika Mji wa Lund, Bara la Ulaya, "ameeleza Prof. Razack
Amesema watafiti kutoka katika mataifa hayo matatu watapata nafasi ya kueleza ni namna gani siasa na Uongozi inaweza kuathiri utunzaji wa ekolojia na mahusiano yaliyopo baina ya Uongozi uliopo na utunzaji wa mahusiano ya viumbe na wanyama katika mazingira.
"Tanzania inafaidika na tafiti hizi kwani zinafanyika katika hali ya hewa tofauti kwani huu muunganiko utasaidia kupata tafiti zitakazosaidia kutatua migogoro ya kijamii na kiikolojia kupitia mitazamo wa ekolojia ya kisiasa," amesema Prof. Razack
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) , Idara ya jiografia na Stadi za Mazingira Dkt. Mathew Mabele amesema mwaka huu watafiti watapata nafasi ya kuwasilisha matokeo ya tafiti zao bila kusafiri kwenda Ulaya kwani imezoeleka mikutano hii inafanyika Ulaya na inapelekea kuwepo kwa changamoto hasa ya kifedha ama VISA kwa watafiti kutoka Afrika au Asia kuhudhuria.
"Mpangilio wa kuwa na hizi nchi Tatu umetokana na namna ambavyo mikutano ya Kitafiti na Kiakademia mara nyingine zimekuwa ziifanyika katika nchi za Ulaya na washiriki kutoka Ulaya na Amerika wmekuwa wakipata changamoto ya VISA na Fedha sasa mwaka huu tukasema tufanye katika nchi hizi Tatu ili watafiti wapate nafasi ya kuwasilisha matokeo yao mwenyewe, " amesema Dkt. Mabele
Kwa upande wake Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Virginia nchini Marekani, Prof. James Igoe , amesema ni vyema kuhusisha watu waliopo katika mazingira ya hifadhi ili kusaidia kulinda ekolojia na uhusiano wa wanyama na viumbe pamoja na mazingira.
"utunzaji wa ekolojia na mazingira kwa ujumla ni jambo shirikishi ndio maana changamoto nyingi zinazojitokeza ni kukosekana tu kwa Mawasiliano mazuri ndio maana hata kwenye kushirikiana na Jamii kulinda na kuhifadhi ekolojia zetu ni vyema jamii ikashirikishwa kikamilifu, " @ameeleza Prof. James
No comments:
Post a Comment