SERIKALI imesitisha zoezi la ukaguzi wa risiti za Kielekroniki (EFD) na ritani za kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia mkoa wa kikodi wa Kariakoo, Jijini Dar es Salaam, wakati ukiandaliwa utaratibu mzuri wa utekelezaji wa suala hilo katika Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo.
Hayo yamesemwa kwa niaba ya Serikali, jijini Dodoma, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, wakati akitoa maazimio ya kikao kati ya Viongozi wa Wafanyabiashara Tanzania, Viongozi wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na Taasisi zinazosimamia masuala ya wafanyabiashara, kikao ambacho kiliitishwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na kuhudhiriwa pia na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.
############
 |
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akieleza nia njema ya Serikali katika kuhakikisha kunakuwa na mazingira bora ya ufanyaji biashara nchini, wakati wa kikao kati ya Viongozi wa Wafanyabiashara Tanzania, Viongozi wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na Taasisi zinazosimamia masuala ya wafanyabiashara, jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Jenista Mhagama. |
No comments:
Post a Comment