TANESCO YATEKELEZA AGIZO LA RAIS SAMIA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, June 19, 2024

TANESCO YATEKELEZA AGIZO LA RAIS SAMIA.


Na Carlos Claudio, Dodoma.


Shirika la umeme Tanzania TANESCO limejikita katika kutoa huduma katika mifumo ya kidijitali nchini, kuelekea wiki ya maadhimisho ya utumishi wa umma 2024  imeweza kutekeleza agizo la Rais Dkt.  Samia Suluhu Hassan la mashirika ya umma kujikita katika mifumo hiyo ya kidijitali.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 19, 2024 jijini Dodoma, Afisa huduma kwa wateja wa Shirika la umeme Tanzania TANESCO Fatuma Mohamed amesema wamekuwa kipaumbele katika maonyesho hayo ili kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuyataka mashirika mashirika ya umma kujikita katika huduma za kidijitali.


Amesema TANESCO ikiwa ni shirika la umma limeweza kujikita katika kutoa huduma katika mfumo wa kidijitali kuanzia na mfumo wa kuunganisha umeme pamoja na kuongeza wigo katika matumizi ya TEHAMA kwa upande wa kutoa taarifa kwa jamii.


“TANESCO limejikita pia katika kutoa huduma katika mfumo wa kidijitali tukianzia na mfumo wetu wa kuonganisha umeme wa NIKONECT ambao ni wa kidigitali kwankuunganisha umeme kwa wateja ambapo kwa sasahivi mteja sio lazima afike ofisini ili kupata huduma ya kuonganishiwa umeme, mteja popote alipo akiwa na simu janja ila hata akiwa na simu zile za kitochi anaweza kufanya maombi na anaweza kuonganishiwa umeme bila kufika ofisi za TANESCO,”


Fatuma ameongeza kuwa,“ TANESCO pia imeongeza wigo wa kutumia TEHAMA kwa upande wa kutoa taarifa mbalimbali ambayo tunaiita JISOT ambao ni mfumo mteja anaweza akatoa taarifa kwa njia ya simu janja.” ambapo kwa kupitia namba yetu ile ile ya kutolea taarifa kwenye kituo cha miito ya simu TANESCO ambay


Amesema kwankutumia JISOT taarifa hiyo inatumwa kupitia namba ya kutolea taarifa kwenye kituo cha miito ya simu Tanzania TANESCO ambayo ni 0748550000 ambayo namba hiyo pia inatumika kwa mtandao wa kijamii wa Whatsapp kwa kutuma ujumbe hi au hello.


Aidha amesema faida ya huduma hizo ni kuokoa muda wa mteja kusafiri umbali pamoja na usumbufu wa kutafuta ofisi ili kujipatia huduma lakini pia TANESCO wameweza kupata taarifa kwa haraka kiganjani na urahisi wa kuhudumia mteja kwa uharaka.


Sambamba na hayo Fatuma ameeleza kuwa mfumo wa JISOT unamruhusu mteja kuweza kujihudumia mwenyewe kwa kuuliza maswali au kupitia changamoto atakazozipata kutokana na huduma au hitilafu ya umeme itakayojitokeza.


Shirika la umeme Tanzania TANESCO limekuwa na huduma mbalimbali za kidijitali ikiwemo Whatsapp, Instagram na  (X) Twitter zinazotoa huduma kwa wateja.





No comments:

Post a Comment