Na Carlos Claudio, Dodoma.
Mamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania TIRA imeendelea kutoa elimu kwa jamii kuelekea wiki ya maadhimisho ya utumishi wa umma juu ya umuhimu na madhara ya kutotumia bima, pamoja na kuandaa kanuni na miongozo itakayoleta maelewano katika jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 19, 2024 jijini Dodoma, Meneja uhusiano mamlaka ya usimamizi bima Tanzania TIRA Hadija Maulid amesema katika maonyesho hayo ya ushiriki wa umma wana jukumu la msingi kisheria la kutoa elimu ya bima kwa umma na kupitia majukwaa mbalimbali wanahakikisha elimu hiyo inafikia umma kwa urahisi.
Amesema wamekuwa na majukumu ya kusajili watu wa huduma kwa umma pamoja na kuadaa kanuni na miongozo kwa dhumuni la kuleta maelewano katika soko la bima.
“Mpaka hivi sasa tunavyozungumza mamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania imesajili watoa huduma mbalimbali za bima zaidi ya 1600 ni ongezeko la asilimia nyingi ukilinganisha na takwimu za mwaka 2021, lakini pia hata tunavyozungumza leo hii watumiaji wa huduma za bima wameongezeka kutoka milioni 6 kwa takwimu za mwaka 2021 lakini leo hii tuna watumiaji wa huduma mbali mbali za bima wanaofika zaidi ya milioni 12 ambalo ni ongezeko la takribani asilimia 100,”
“Ujumbe wangu ninaotaka kujulisha watanzania kuwa soko la bima linakuwa, watu wanaelewa umuhimu wa bima lakini pamoja na hayo bado tunatoa rai kwa wananchi kutumia huduma mbali mbali za bima ili kuweza kujikinga na majanga ambayo yasiyotarajiwa.” amesema Hadija.
Aidha ameeleza kuwa TIRA wapo kwa jukumu la kusimamia haki za wateja wa bima hivyo mteja wabima anapopata changamoto yoyote wapo kwaajili ya kusimamia hilo na kuhakikisha kwamba haki zake za msingi zinapatikana kwa muujibu wa taratibu ambazo zipo kwenye miongozo ambayo imetungwa na kusimamiwa.
Hata hivyo amebainisha kuwa TIRA imekuwa ikitoa elimu kupitia kanda zake 10 ambazo ni magharibi ambayo ofisi ipo Tabora, kanda ya mashariki ambayo ofisi yake ipo Dar Es Salaam inayohudumia Morogoro na Pwani, kanda ya kusini ambayo ofisi yake ipo Lindi inayohudumia Mtwara na mikoa ya kusini, kanda ya Zanzibar inayohudumia mikoa ya Zanzibar pamoja na kanda ya Pemba kwa lengo kuhakikisha zinahudumia mikoa yote kwa kutoa elimu ya bima kwa wananchi.
Kwa upande wake meneja usimamizi wa utekelezaji wa sheria Okoka Mgavilenzi amesema bima ni kinga dhidi ya majanga hivyo binadamu hawezi kuepuka majanga kwa kuwa yapo majanga ya aina mbali mbali ikiwa mafuriko, hali ya hewa, kilimo, uvuvi, ufugaji pamoja na magonjwa ya mifugo.
Amesema mtanzania hapaswi kunun’gunika kwa kudhulumiwa, kukosa haki zake za msingi ikiwemo kucheleweshewa madai pamoja na kuhudumiwa kwa lugha isiyofaa kwa kuwa msaada wake upo mamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania TIRA.
“Kwa sasahivi kuna jambo jema serikali imeamua kulifanya la kuhakikisha kwamba tunapeleka bima ya afya kwa wananchi wote haijalishi upo mjini au kijijini wote inapaswa kuwa na bima ya afya kwaajili ya kuhakikisha kwamba hayupo mtanzania anayeteteleka uhai wake kwaajili ya kukosa matibabu,”
Mgavilenzi ameongeza kuwa,“ Tumezungumza hapa habari za kilimo, tumesha anza skimu ya bima za kilimo na tunavyofahamu kilimo mara nyingi hakifanyiki kwa kiwango kikubwa sana maeneo ya mijini, kilimo kinafanyika hasa kwa maeneo ya vijijini ambapo tunasema wananchi labda hawafikiwi labda na elimu.
No comments:
Post a Comment