WANANCHI 231 WANUFAIKA NA BIMA YA AFYA BURE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, June 22, 2024

WANANCHI 231 WANUFAIKA NA BIMA YA AFYA BURE


Wazee, wajane na wasichana waliopata ujauzito shuleni wanufaika na mpango wa kusaidia watu wenye mahitaji maalumu unaotekelezwa na Triprecy Initiative Foundation katika wilaya ya Chamwino, Dodoma.

Akizungumza na OKULY BLOG Mkurugenzi wa Triprecy Initiative Foundation Bwana Benson Magoti amesema kati yao walionufaika na mpango wa bima bure ni wajane 40, wazee 61 na wasichana waliopata ujauzito shuleni 90 huku 13 kati yao wanaendelea na masomo.

Aidha amesema kwa wasichana wanapewa bima yenye kifurushi cha mama na mtoto ili kuwawezesha kuendelea na masomo au kuendelea na shughuli nyingine huku wakiwa na uhakika wa kupata huduma ya matibabu katika vituo vya kutolea huduma ya afya.

Hayo yamejili katika maonyesho ya Idodomia International Expo yanayoendelea katika viwanja vya shule ya sekondari Dodoma mkabala na bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Idodomia Expo imeandaliwa na Triprecy Initiative foundation, ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma, Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) taasisi za mbalimbali za serikali pamoja na wadau wengine.

No comments:

Post a Comment