WAZIRI MHAGAMA AIPONGEZA THPS KUWEKEZA KATIKA HUDUMA ZA TIBA KWA WARAIBU WA DAWA ZA KULEVYA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, June 30, 2024

WAZIRI MHAGAMA AIPONGEZA THPS KUWEKEZA KATIKA HUDUMA ZA TIBA KWA WARAIBU WA DAWA ZA KULEVYA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia kabla ya kumkabidhi cheti cha Ushiriki katika maonesho ya kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya duniani yaliyofanyika kuanzia Juni 27 - 30,2024 katika viwanja vya Nyamagana Jijini Mwanza
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati alipotembelea Banda la THPS kwenye maonesho ya kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya duniani yaliyofanyika kuanzia Juni 27 - 30,2024 katika viwanja vya Nyamagana Jijini Mwanza
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia cheti cha Ushiriki katika maonesho ya kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya duniani yaliyofanyika kuanzia Juni 27 - 30,2024 katika viwanja vya Nyamagana Jijini Mwanza - Picha na Kadama Malunde

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama amelipongeza Shirika Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa namna linavyoshirikiana na Serikali na wadau mbalimbali katika kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwekeza katika huduma ya tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya (MAT).

 Mhe. Mhagama ametoa pongezi hizo Jumamosi Juni 29,2024 alipotembelea Banda la THPS ambao ni miongoni mwa wadau wanaoshiriki maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya kupiga vita dawa za kulevya duniani katika viwanja vya Nyamagana  Jijini Mwanza yakiongozwa na Kauli mbiu “Wekeza kwenye kinga na tiba dhidi ya dawa za kulevya”.

Akiwa katika banda la THPS, Mhe. Mhagama ameshuhudia namna THPS inavyotoa elimu kuhusu huduma za tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya zinazotolewa kwenye vituo vya Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (Medically Assisted Therapy – MAT).

Mhe. Mhagama ameipongeza THPS kwa namna inavyoshirikiana na Serikali kutoa huduma za tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya nchini.

"Kwa pamoja tunaweza kishinda vita dhidi ya matumizi na usafirishaji wa dawa za kulevya", amesema Mhe. Mhagama.

Awali, THPS ilishiriki katika mdahalo wa Kitaifa kuhusu jitihada mbalimbali za wadau na Serikali katika kupambana na matumizi na usafirishaji wa dawa za kulevya.

Katika mdahalo huo, Mhe. Mhagama amewapongeza wadau wote walioshiriki kwa kusimama bega kwa bega na Serikali katika vita hii.

Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia amesema
THPS imeungana na Serikali na wadau wengine katika kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwekeza katika huduma ya tiba kwa waraibu (MAT) na huduma za kinga, matunzo na matibabu ya maambukizi ya VVU na Kifua kikuu.

"Tumefanikiwa kuandikisha watumiaji wa dawa za kulevya 2,442 katika mpango wa MAT na kati yao 1,426 bado wanaendelea na matibabu",amesema Dkt. Redempta.

Amesema Mradi wa Afya Hatua umekuwa ukiziwezesha Asasi za Kiraia (AZAKI) katika mikoa ya Tanga na Pwani katika utambuzi wa waraibu wa dawa za kulevya, kuwapatia elimu na kuwaunganisha na huduma za MAT. 

THPS inatekeleza afua ya huduma ya Tiba kwa waraibu (MAT) katika mikoa ya Pwani na Tanga kupitia mradi wa Afya Hatua inaoutekeleza kwa ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) kupitia Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (US. CDC).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akizungumza wakati akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia cheti cha Ushiriki katika maonesho ya kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya duniani yaliyofanyika kuanzia Juni 27 - 30,2024 katika viwanja vya Nyamagana Jijini Mwanza - Picha na Kadama Malunde

Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia akimwelezea Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama namna THPS inavyoshirikiana na Serikali na wadau mbalimbali katika kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwekeza katika huduma ya tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya (MAT).
Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia akimwelezea Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama namna THPS inavyoshirikiana na Serikali na wadau mbalimbali katika kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwekeza katika huduma ya tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya (MAT).
Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia akimwelezea Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama namna THPS inavyoshirikiana na Serikali na wadau mbalimbali katika kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwekeza katika huduma ya tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya (MAT).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati alipotembelea Banda la THPS kwenye maonesho ya kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya duniani yaliyofanyika kuanzia Juni 27 - 30,2024 katika viwanja vya Nyamagana Jijini Mwanza
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati alipotembelea Banda la THPS kwenye maonesho ya kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya duniani yaliyofanyika kuanzia Juni 27 - 30,2024 katika viwanja vya Nyamagana Jijini Mwanza
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akisikiliza maelezo kuhusu huduma za tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya (MAT) zinazotolewa kupitia THPS wakati alipotembelea Banda la THPS kwenye maonesho ya kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya duniani yaliyofanyika kuanzia Juni 27 - 30,2024 katika viwanja vya Nyamagana Jijini Mwanza

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akisikiliza maelezo kuhusu huduma za tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya (MAT) zinazotolewa kupitia THPS wakati alipotembelea Banda la THPS kwenye maonesho ya kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya duniani yaliyofanyika kuanzia Juni 27 - 30,2024 katika viwanja vya Nyamagana Jijini Mwanza

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wanufaika wa huduma za tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya (MAT) zinazotolewa kupitia THPS wakati alipotembelea Banda la THPS kwenye maonesho ya kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya duniani yaliyofanyika kuanzia Juni 27 - 30,2024 katika viwanja vya Nyamagana Jijini Mwanza.
Afisa Mradi wa THPS anayeshughulikia Huduma za MAT katika Mkoa wa Pwani, Dkt. Joshua Mharagi akielezea namna wanavyotoa huduma ya tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya (MAT)
kwenye Mdahalo wa Kitaifa Kujadili Madhara ya Dawa za Kulevya uliofanyika leo Jumamosi Juni 29,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza kwenye Mdahalo wa Kitaifa Kujadili Madhara ya Dawa za Kulevya uliofanyika leo Jumamosi Juni 29,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda akizungumza kwenye Mdahalo wa Kitaifa Kujadili Madhara ya Dawa za Kulevya uliofanyika leo Jumamosi Juni 29,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo akizungumza kwenye Mdahalo wa Kitaifa Kujadili Madhara ya Dawa za Kulevya uliofanyika leo Jumamosi Juni 29,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo akizungumza kwenye Mdahalo wa Kitaifa Kujadili Madhara ya Dawa za Kulevya uliofanyika leo Jumamosi Juni 29,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo  akizungumza kwenye Mdahalo wa Kitaifa Kujadili Madhara ya Dawa za Kulevya uliofanyika leo Jumamosi Juni 29,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo  akizungumza kwenye Mdahalo wa Kitaifa Kujadili Madhara ya Dawa za Kulevya uliofanyika leo Jumamosi Juni 29,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Afisa Mradi wa THPS anayeshughulikia Huduma za MAT katika Mkoa wa Pwani, Dkt. Joshua Mharagi akielezea namna wanavyotoa huduma ya tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya (MAT)
kwenye Mdahalo wa Kitaifa Kujadili Madhara ya Dawa za Kulevya uliofanyika leo Jumamosi Juni 29,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

No comments:

Post a Comment