AFISA MKUU WA HAMAS AUAWA HUKU ISRAEL IKIWAAMURU UPYA WATU KUHAMA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, July 8, 2024

AFISA MKUU WA HAMAS AUAWA HUKU ISRAEL IKIWAAMURU UPYA WATU KUHAMA.

Kifo cha Al-Ghussein hakichukuliwi kuwa pigo kwa Hamas kijeshi.

Afisa mkuu wa utawala wa Hamas alikuwa miongoni mwa watu wanne waliouawa katika shambulizi la anga la Israel lililofanyika katika shule moja katika mji wa Gaza, duru za Palestina zinasema.


Afisa mmoja wa eneo hilo ameiambia BBC kwamba Ehab Al-Ghussein aliteuliwa kusimamia maswala ya serikali ya Hamas katika mji wa Gaza na kaskazini mwa Gaza miezi mitatu iliyopita.


Jeshi la Israel linasema kuwa lilifanya shambulizi katika eneo la jengo la shule katika mji wa Gaza ambapo linasema "magaidi walikuwa wakiendesha shughuli zao na kujificha".


Linasema kwamba lilichukua hatua hiyo ili kupunguza hatari ya kuwadhuru raia.


Walioshuhudia wanasema shambulio hilo lililenga Shule iliyo karibu na Kanisa la Holy Family, magharibi mwa mji wa Gaza. Idadi kubwa ya watu walikuwa wamejihifadhi katika jengo hilo, BBC inafahamu.


Shambulio hilo la anga ulilenga vyumba viwili vya madarasa kwenye ghorofa ya chini, walisema.


Ehab Al-Ghussein aliwahi kuwa naibu waziri wa kazi katika utawala wa Hamas na kabla ya hapo alikuwa msemaji wa wizara ya mambo ya ndani.


Kifo chake hakichukuliwi kuwa pigo kwa Hamas kijeshi, lakini alichukuliwa kuwa mtu muhimu katika utawala wa Hamas.


Watu wengine wengi wameuliwa katika utawala wa Hamas katika muda wa miezi tisa iliyopita.

No comments:

Post a Comment