DKT. JAFO ATAKA KASI UJENZI JENGO LA OFISI YA MAKAMU WA RAIS - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, July 2, 2024

DKT. JAFO ATAKA KASI UJENZI JENGO LA OFISI YA MAKAMU WA RAIS


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la utawala la Ofisi ya Makamu wa Rais unaondelea katika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma leo tarehe 02 Julai, 2024.

Pamoja na kutembelea maeneo mbalimbali ya jengo hilo, pia amekagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Muungano (Makavazi) kinachojengwa katika jengo hilo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Waziri Jafo amemtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi ambaye ni Kampuni ya SUMA JKT kuongeza kasi katika ujenzi ili likamilike kwa wakati.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi akimuelezea Waziri amesema makavazi hayo yakuwa katika namna mbalimbali zikiwemo kwa mfumo wa elektroniki na nyaraka ngumu.

Hivyo, jingo hilo litakapokamilika pamoja na kuwawezesha watumishi kufanya kazi kwa ufanisi lakini pia kitasaidia kuhifadhi kumbukumbuku muhimu za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa vizazi vyote.

Aidha, katika ziara Mhe. Dkt. Jafo aliambatana na baadhi ya wakurugenzi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.

No comments:

Post a Comment