HAKIKISHA MNAZINGATIA SHERIA, TARATIBU NA KANUNI (STK) - ABDULLA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, July 12, 2024

HAKIKISHA MNAZINGATIA SHERIA, TARATIBU NA KANUNI (STK) - ABDULLA.

 


Na Carlos Claudio, Dodoma.


Wataalam wa TEHAMA waliopata ufadhili kupitia mradi wa Tanzania ya Kidigitali wamepewa vyeti na kutia saini ya makubaliano kama mkataba wa kuitumikia serikali baada ya kumaliza masomo yao.


Akizungumza leo Julai 12, 2024 jijini Dodoma katika hafla hiyo Katibu Mkuu wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Khamis Abdulla amesisitiza kwa wanufaika wa mradi huo kuzingatia sheria, taratibu na kanuni kipindi wanapoenda kusoma nje ya nchi.


“Kabla haujaondoka fanya mawasiliano na ubalozi kwamba unaenda kwenye nchi fulani, na ukifika pale kabla haujafanya jambo lolote nenda ubalozini kwasababu lolote likitokea huko sehemu pa kukimbilia pekeyake ni ubalozi,”


“Weledi mkubwa kabisa umefanyika ili kupata watu 30 wanaotoka kwenye wizara mbalimbali na taasisi ndani ya serikali, watumishi hawa 30 watakwenda kusoma nje ya nchi kwenye fani zinazohusiana na masuala ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano zinazoibukia kama maeneo ya akili bandia , usalama mtandao na mambo mengine.” amesema Abdulla.


Amesema kada hiyo ni tatizo kwa kuwa ni teknolojia mpya ambazo zinaibukia hivyo anatarajia wanufaika wa mradi huo wataenda kujifunza kwa bidii huku wakizingatia sheria, taratibu pamoja na kanununi.


Abdulla amesema kuwa ufadhili huo unatolewa kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali ambapo kwani kwa sasa TEHAMA ni nyenzo muhimu na wezeshi katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa idara ya DIASPORA kutoka wizara ya mambo ya nje Salvatory Mbilinyi amesisitiza wanufaika wa mradi huo kutii na kufuata sheria za nchi pamoja na vyuo ambavyo wanaenda ili waweze kutimiza malengo yao kwa manufaa ya taifa, familia pamoja wao binafsi.


Mbilinyi amehimiza wanufaika wa mradi huo waweze kuwa wavumilivu na changamoto zozote kipindi wapo masomoni pamoja na kulinda tamaduni waliyojengewa na taifa kwa kuzingatia maadili ya kitanzania na siyo kujisahau wanapokutana na tamaduni za nje ya nchi.


Nae meneja biashara kutoka CRDB Joseph Mhagama amesema hao kama taasisi wanampango madhubuti wa kuwasaidia watu wote ambao wapo katika kundi la DIASPORA katika kutatua changamoto za fedha kipindi wapo ughaibuni.


“Kwenye huduma za kifedha sisi kama CRDB sasa hivi tuna amini nyinyi kama wanufaika mnawekuwa na akaunti zenu za kawaida, lakini kwasababu ya mabadiliko unahitaji kuwa na akaunti maalum ambayo tunaiita akaunti ya Tanzanite.”


Mhagama ameongeza kuwa, “ Tunawapa akaunti ya Tanzanite kwa ajili ya kuitangaza nchi pamoja na huduma za kipekee ambazo mtaweza kuhudumiwa kupitia mawakala wetu ambao watakuwa nje ya nchi ulipo, kwa hiyo niwape habari njema popote pale utakapoenda kuna wakala atayeweza kukuhudumia kwa chochote utakachokuwa unahitaji kuhusiana na huduma za kibenki.”









No comments:

Post a Comment