HATUNA HURUMA NA WADANGANYIFU KWENYE MITIHANI- WAZIRI MKENDA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, July 13, 2024

HATUNA HURUMA NA WADANGANYIFU KWENYE MITIHANI- WAZIRI MKENDA


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema katika Chuo Kikuu ukikamatwa umedanganya kwenye mtihani adhabu yake ni kufukuzwa chuo moja kwa moja, na yeye kama Waziri mwenye dhamana hatoingilia mamlaka za Vyuo Vikuu zinapochukua hatua hizo kulinda mitihani.

Kauli hiyo ameitoa leo Julai 12, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu tuhuma zinazorushwa kwenye mitandao na baadhi ya vyombo vya Habari kwamba kuna udanganyifu kwenye Vyuo Vikuu hasa kwenye masuala ya mitihani.


‘’Kila tunaposikia tuhuma tunachukulia kama jambo zito sana, kulikuwa na dalili kama hizo katika mitihani ya darasa la saba, kidato cha Nne na Sita, na tulichukua hatua kali, ambazo kwa bahati mbaya zinaumiza hata maslahi ya baadhi ya wawekeza katika sekta ya elimu’’ Alisema Mkenda. 

Ameongeza kuwa suala la udanganyifu katika mitihani lina madhara makubwa kwani linaondoa usawa, na kwamba Serikali inataka Wanafunzi wanapofanya mitihani wote wapimwe kwa usawa na haki, isitokee mmoja anafanya mtihani kwa udanganyifu na kufaulu wakati mwingine ana tumia juhudi zake.

‘’Tukiruhusu udanganyifu wowote katika elimu, ngazi yoyote ya elimu, tunakuwa tunalea na kufundisha rushwa kwa Wanafunzi wetu, tutaendelea kusimamia uadilifu katika mitihani". Alisema Mkenda.

Amewahakikishia Watanzania wote kwamba Vyuo yetu vinazingatia sana maadili hasa katika masuala ya mitihani na weledi kuhakikisha tunatoa degree kwa mujibu wa taratibu zinazokubalika katika taaluma yetu nchini.

No comments:

Post a Comment