HATUTAKI NYONGEZA YA MSHAHARA- RAIS RUTO. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, July 4, 2024

HATUTAKI NYONGEZA YA MSHAHARA- RAIS RUTO.

 


Rais wa Kenya William Ruto ametaka kuangaliwa upya mara moja kwa mapendekezo ya nyongeza ya mishahara kwa maafisa wa serikali

Hili huenda ndilo kubwa zaidi ambalo limetokana na shinikizo ya wananchi na hasa kutokana na maandamano ya hivi karibuni .


Ndio hatua muhimu inayoonekana kujibu lalama za wengi nchini humo ambazo zinahusu watu katika nyadhifa kuu serikalini kuwatwika mamilioni ya wananchi mzigo wa kugharamia mishahara yao ya juu na maisha ya kifahari. 


Kando na rais William Ruto kulazimika kuufutilia mbali mswada wa fedha uliowasha maandamano hayo,hatua hii ya hivi punde inaingia katika orodha ya 'ushindi' wa waandamanaji.


Ingekuwa ajabu iwapo wabunge,maseneta na rais wangesalia kimya na kuendelea na mambo kama kawaida iwapo notisi hiyo ya SRC ya kuwaongeza maafisa wakuu serikalini mishahara ingetekelezwa.


Viongozi wengi kwa kauli moja waliikemea hatua hiyo ya SRC kutoa notisi ya nyongeza ya mishahara wakati huu hasa baada ya maandamano ya wanancha na wakikariri msimamo wa rais Ruto kwamba uchumi kwa wakati huu hauna nguvu kuweza kubeba mzigo wa nyongeza hiyo.


Kenya kwa sasa inatumia zaidi ya shilingi trilioni moja kuwalipa wafanyakazi wa umma, na kuna ongezeko la shilingi bilioni 29 la fedha zinazolipwa kama mishahara kwa watumishi wa umma licha ya tume ya mishahara kuzuia nyongeza ya hivi punde.

No comments:

Post a Comment