'MATUNDA YA MAANDAMANO YA VIJANA WA KENYA NA MATUMAINI YA MAGEUZI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, July 4, 2024

'MATUNDA YA MAANDAMANO YA VIJANA WA KENYA NA MATUMAINI YA MAGEUZI.



Mwanzoni walipuuzwa kama vijana wavivu ambao muda wao mwingi waliiutumia katika mitandao ya kijamii.


Wakati walipoamua kutekeleza hatua yao ya kwenda barabarani ili kulalamikia mswada wa fedha uliokuwa ukipendekeza nyongeza ya ushuru kwa bidhaa mbalimbali,wengi waliwapuuza na hawakujua athari za walichokianzisha.


Lakini sasa ni wazi kwamba licha ya maandamano ya vijana wa Kenya wa kizazi cha Gen Z kuingiliwa na makundi ya uhalifu na magenge ya uporaji-kuna mazuri ambayo yametokea kwa sababu ya hatua ya vijana hao.


Serikali na uongozi wa nchi sasa unaonekana kuchukua kila hatua kwa uangalifu. Miongoni mwa mambo ambayo huenda yaliwashtua wengi,ni viongozi wa kisiasa kujitokeza na kukataa nyongeza ya mishahara iliyopendekezwa na Tume ya mishahara ya nchi hiyo SRC.

No comments:

Post a Comment