JD VANCE: MGOMBEA MWENZA WA TRUMP AAPA KUWAPIGANIA WAMAREKANI WALIOSAHAULIKA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, July 18, 2024

JD VANCE: MGOMBEA MWENZA WA TRUMP AAPA KUWAPIGANIA WAMAREKANI WALIOSAHAULIKA.


Mgombea mwenza aliyeteuliwa na Donald Trump aliapa katika hotuba yake ya kwanza kuwapigania Wamarekani wa tabaka la wafanyakazi ambao alidai kuwa "wamewekwa pembeni na kusahauliwa" na Wanademocrats.


Akijitambulisha kwa mamilioni ya Wamarekani waliokuwa wakitazama kupitia runinga wakiwa majumbani, seneta huyo wa Ohio kwa unyenyekevu kutoka Midwest alishambulia kwa maneno wale ambao "siasa ndio kazi zao" kama Rais Joe Biden.


Alihoji katika hotuba yake kwenye Kongamano la Kitaifa la Republican huko Milwaukee, Wisconsin, kwamba Trump alikuwa "tumaini bora la mwisho" kwa Wamarekani.


Trump na mgombea mwenza wake wataingia kwenye kinyang’anyiro cha kutafuta tikiti ya kuingia Ikulu, wakishindana na mgombea wa Democratic ambaye kwa sasa ni Bw Biden na makamu wake, Kamala Harris, katika uchaguzi wa Novemba.


Akaunti ya Bw Biden kwenye mtandao wa X, ilimjibu Bw Vance Jumatano usiku, kuhusu misimamo yake katika masuala ya uavyaji mimba na Ukraine.


Bw Vance, 39, anatumai kuwa mmoja wa makamu wa rais wachanga zaidi katika historia ya Marekani.

No comments:

Post a Comment