UJERUMANI INAPANGA KUPUNGUZA NUSU YA MSAADA WA KIJESHI KWA UKRAINE. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, July 18, 2024

UJERUMANI INAPANGA KUPUNGUZA NUSU YA MSAADA WA KIJESHI KWA UKRAINE.


Ujerumani inapanga kupunguza nusu ya msaada wa kijeshi kwa Ukraine mwaka ujao, kutoka karibu €8bn (£6.7bn; $8.7bn) hadi karibu €4bn, kulingana na rasimu ya bajeti iliyoidhinishwa na serikali.


Waziri wa Fedha Christian Lindner alisema ufadhili wa Ukraine ulikuwa "salama kwa mustakabali wa baadaye" kutokana na mpango wa kundi la G7 la mataifa tajiri wa kupata $50bn kutokana na riba ya mali ya Urusi iliyozuiliwa.


Ujerumani ni mfadhili mkuu wa pili wa kijeshi wa Ukraine baada ya Marekani. Mnamo 2024, bajeti ya Berlin kwa Kyiv imepangiwa kuwa karibu € 7.5bn.


Kupunguzwa kwa misaada iliyopangwa kunawadia huku kukiwa na hofu nchini Ukraine na kwa washirika wake wa Ulaya kwamba ufadhili wa Marekani unaweza kupunguzwa au hata kusimamishwa ikiwa Donald Trump atashinda urais katika uchaguzi wa Novemba.


Rais wa Urusi Vladimir Putin alianzisha uvamizi dhidi ya Ukraine mnamo Februari 2022.

No comments:

Post a Comment