MSHAMBULIAJI WA TRUMP ALIONEKANA KAMA TISHIO KABLA YA KUFYATUA RISASI LAKINI ALIPOTEA KWENYE UMATI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, July 18, 2024

MSHAMBULIAJI WA TRUMP ALIONEKANA KAMA TISHIO KABLA YA KUFYATUA RISASI LAKINI ALIPOTEA KWENYE UMATI.

 


Mtu ambaye angemwua Donald Trump aliripotiwa kama mwenye "kutiliwa mashaka" na Huduma Maalum ya Usalama hadi saa moja kabla ya kuanza kumfyatulia risasi Trump lakini akapotea kwenye umati wa watu, wabunge wamearifiwa na maafisa wa usalama.


Maafisa wa usalama pamoja na Huduma Maalum ya Usalama walitoa taarifa kidogo kwa Bunge na Seneti ya kile kilichotokea wakati wa shambulizi hilo lililotokea kwenye mkutano wa Trump huko Pennsylvania.


Seneta wa Wyoming John Barrasso alisema Huduma Maalum ya Usalama iliwaambia kwamba walimwona mshambuliaji saa moja kabla ya shambulio hilo, lakini akawapotea machoni.


"Alitambuliwa kama anayetiliwa mashaka kwa sababu [alikuwa na] chombo cha kukadiria umbali wa kitu hasa kwa matumizi na kamera au bunduki na mkoba mgongoni. 


Na hii ilikuwa zaidi ya saa moja kabla ya ufyatuaji wa risasi kutokea," aliiambia Fox News.


"Kwa hiyo, unaweza kutafakari, kwa muda wa saa nzima, usimpoteze mtu huyo machoni."


Ilifichuliwa wakati wa kikao hicho kwamba mtu huyo alikuwa ametembelea eneo alilotekeleza shambulizi kabla ya mkutano na pia, aliwahi kutafuta kwenye simu yake, dalili za ugonjwa wa mfadhaiko, afisa mwingine aliiambia CBS News, mshirika wa habari wa BBC.


Aidha, mshambuliaji huyo aliwahi kutumia simu yake kutafuta picha za Donald Trump na Joe Biden.

No comments:

Post a Comment