Miradi hiyo ambayo Mwenge umepitia ni pamoja na Duka la vijana wis kwa ntis,mradi wa Maji Hachwi,mradi wa barabara Gubali Bolisa-Iboni,Bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum Iboni,mradi wa msitu miombo Hachwi na mradi wa zahanati ya Choka,
Akiwa katika mradi wa Maji Hachwi Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka huu Ndugu Godfrey Mnzava amewahakikishia wananchi wa mtaa wa Hachwi kuwa mradi wa maji unaoendelea utakamilika na kutoa huduma kwa wananchi kwa kuwa upo asilimia 90 ya utekelezaji wake.
Hata hivyo Baada ya kuongea na wananchi wa mtaa huo waliofika kuupokea Mwenge wa Uhuru ameweka jiwe la Msingi katika mradi wa maji Hachwi ambao umegharimu shilingi milioni 800 zilizotolewa na serikali kuu.
Pia mradi huo unatarajia kuwanufaisha wananchi zaidi ya 2000 wa mtaa wa Hachwi.
Katika hatua nyingine akiwa katika Mradi wa msitu wa miombo kiongozi huyo wa mbio za mwenge amewataka wananchi kuendelea kutunza Mazingira na kuyahifadhi vizuri.
"Shughuli zetu za Kilimo ambazo hazizingatii uendelevu na uhifadhi mzuri wa Mazingira imeleta changamoto katika Mazingira yetu"
Shughuli za ufugaji, watu wanafuga mifugo bila kuzingatia tija wanazururisha mifugo na yenyewe pia imeleta changamoto kwenye Mazingira"amesema
Akitoa salaam za Jimbo la Kondoa Mjini katika eneo la mradi wa Maji Hachwi Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Ally Makoa amemshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea fedha za mradi huo kwa kuwa wananchi walikuwa wakipata tabu ya maji kwa kipindi kirefu.
(Imeandikwa na Manase Madelemu
No comments:
Post a Comment