TAMASHA LA USAMBARA TOURISM FESTIVAL LASOGEZWA MBELE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, July 20, 2024

TAMASHA LA USAMBARA TOURISM FESTIVAL LASOGEZWA MBELE


Na Ashrack Miraji, Lushoto Tanga.

Mkuu wa wilaya ya Lushoto,Mkoani Tanga, Jafar kubecha amewaomba radhi wananchi na wageni wote waliotarajia kuja kwenye tamasha la  kitalii la "Usambara Tourism Festival" lenye lengo la kukuza uchumi hasa kwenye sekta ya utalii wilayani hapo.


Kubecha amesema tamasha hilo ambalo lilipagwa kufanyika  Julai  25-27 mwaka huu, limesogezwa mbele kutokana sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao, hivyo tamasha hilo litafanyika Septemba 6 - 7  mwaka huu.


"nitumie fulsa hii kuwapa pole wananchi na wageni wetu ambao tuliwatarajia kushiriki kwenye tamasha letu kuja kujionea vivutio mbalimbali vya kitalii na majengo makubwa ambayo yalijegwa na mjerumani hususani jengo la Mkuu wa Wilaya ya Lushoto" alisema Kubecha.

No comments:

Post a Comment