Usher alitoa hotuba ya hisia alipopokea tuzo ya mafanikio ya maisha yake katika Tuzo za BET siku ya Jumapili.
Mwimbaji-mtunzi wa nyimbo aliwaambia watazamaji wakati akipokea tuzo hiyo kwamba "kufika hapa kwa hakika haikuwa rahisi, lakini imekuwa na thamani yake".
Usher mwenye umri wa miaka 45 anafahamika zaidi kwa vibao vikiwemo Yeah! na You make me wanna.
Usher pia alitwaa tuzo ya msanii bora wa R&B na hip-hop kwenye tamasha hilo.
Alifungua hotuba kwa muda wa dakika 15 kwa kusema: "Tuzo hii ya mafanikio ya maisha, sijui, jamani, ni mapema sana kuipokea? Kwa sababu bado ninakimbia kama nilivyofanya nilipokuwa na umri wa miaka minane.”
Mwimbaji aliendelea kuzungumza kuhusu baba yake kuacha familia yake alipokuwa mtoto.
"Nilikuwa nikijaribu kuelewa jina hili ambalo mwanaume alinipa ambalo halikudumu kwa sababu hakunipenda," alisema. "Lazima uwe na moyo wa kusamehe ili kuelewa mitego na magumu ya kweli ya mtu mweusi Marekani na baba yangu, alikuwa zao la hilo."
Pia alitafakari maana ya sasa kuwa baba mwenyewe. “Huu ni mwaka wa baba. Simama kwa ajili ya binti zako na watoto wako na uongoze," aliwaambia watazamaji katika ukumbi wa michezo wa Peacock huko Los Angeles. "Ni muhimu kuelewa kwamba baba ni muhimu sana.
"Kwa akina baba wote usiku wa leo nyumbani au kwenye hadhira ningependa ninyi nyote msimame kwa sekunde mbili tu kwa ajili yangu.
Wanaume kadhaa kwenye hadhira waliposimama, Usher alisema: "Hatuna nafasi ya kusema vya kutosha, kwa hivyo hii ni ya wanaume wote huko nje, majenerali wa watoto wao. na motisha kwa viongozi wetu weusi wa baadaye, vijana."
No comments:
Post a Comment