KENYA KUKOPA ZAIDI BAADA YA MUSWADA WA FEDHA KUGONGA MWAMBA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, July 1, 2024

KENYA KUKOPA ZAIDI BAADA YA MUSWADA WA FEDHA KUGONGA MWAMBA.

 


Rais wa Kenya William Ruto anasema nchi italazimika kukopa zaidi ili kuendelea kuendesha serikali kufuatia kukataliwa kwa muswada wa fedha ambao haukupendwa na watu wengi ambao ungeongeza fedha zaidi za ushuru. 


Rais alisema ataondoa muswada huo wenye utata wa nyongeza ya ushuru Jumatano iliyopita baada ya maandamano mabaya ambayo yalisababisha sehemu ya jengo la bunge kuchomwa moto. 


Lakini Jumapili alisema kutupilia mbali mswada huo kumeirudisha nchi nyuma miaka miwili, kwani alieleza ugumu wa kutoweza kuongeza ushuru wa ziada huku ikikabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni. 


Alisema hii ina maana kwamba Kenya italazimika kukopa shilingi trilioni moja ($7.6bn; £6.1bn) "ili tu kuweza kuendesha serikali yetu".


Hili ni ongezeko la 67% zaidi ya kilichokuwa kimepangwa. Lakini pia alisema anazingatia kubana matumizi katika serikali nzima, ikiwa ni pamoja na ofisi yake mwenyewe, na pia kupunguza mgao kwa idara ya mahakama na serikali za kaunti. 


Waandamanaji wengi walipinga kuongezwa kwa ushuru kwa kusema kuwa pesa za ziada zingepotea.


Kulingana na rais, hatua zilizopendekezwa za ushuru zilikuwa sehemu ya juhudi za kupunguza mzigo wa deni wa zaidi ya $80bn (£63bn). 


Takribani 60% ya mapato yanayokusanywa nchini Kenya huenda kwenye kulipia deni. "Nimekuwa nikifanya kazi kwa bidii kuiondoa Kenya kutoka kwenye mtego wa madeni... Ni rahisi kwetu, kama nchi, kusema: 'Hebu tukatae muswada wa fedha.' 


Ni sawa na nimesema tutaondoa muswada wa fedha, lakini itakuwa na madhara makubwa,” rais alisema alipokuwa akizungumza na wanahabari Jumapili usiku. 


Bw Ruto alisema kukataliwa kwa bajeti hiyo kutaathiri ajira kwa walimu 46,000 wa shule za msingi na sekondari ambao wamekuwa kwenye mikataba, pamoja na utoaji wa huduma za afya.

No comments:

Post a Comment