Kiwanda hiki kimeanza uzalishaji wa sukari rasmi Julai 1, 2024 na kina uwezo wa kuzalisha Tani 50,000 za sukari kwa mwaka na kinazalisha Sukari ya Majumbani (Brown Sugar) na pia kinatarajiwa kuzalisha Sukari ya Viwandani (Industrial Sugar) kwa mwaka 2024/2025
Kiwanda hiki kinamilikiwa na Kampuni Hodhi ya Mkulazi ambayo Kampuni hii inamilikiwa kwa ubia kati ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Magereza (SHIMA).
No comments:
Post a Comment