Katika kukabiliana na Changamoto ya upungufu  wa madawati katika halmashauri ya wilaya ya Chemba  Mkoani Dodoma Mbunge wa Jimbo la Chemba Mohamed Monni amekabidhi madawati 200  kwa shule sita za msingi  Miongoni mwa shule hizo ni  pamoja na mapango, Chinika, kelema kuu, paranga ,Rofati  na Chukuruma
Mbunge huyo amekabidhi Madawati hayo leo Alhamisi  Agosti 8,2024 wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo.
Akikabidhi madawati hayo yenye thamani ya shilingi milioni 20 Mbunge Monni  amesema  madawati hayo yatasaidia kupunguza  uhaba huo wakati serikali ikifanya jitihada za kumaliza changamoto hiyo
Amesema madawati hayo yatakuwa  chachu kuongeza  ufaulu kwa wananfunzi huku akiwataka  wazazi, walezi  kushirikiana na walimu katika kuwahamasisha wanafunzi kusoma kwa bidii ili kuweza kujikwamuwa kiuchumi  na kuondokana na wimbi la umaskini katika jamii ya watu wa Chemba
“Leo nimekabidhi madawati 200 kwa ajili ya shule sita za msingi katika halmashauri ya wilaya ya Chemba pamoja najitihada za serikali kupambana na kuboresha miundombinu ya elimu niwaase vijana wangu msome kwa bidii,elimu ni msingi wa maisha lakini pia ndiyo chanzo kikuu cha maarifa.





No comments:
Post a Comment