Na Mwandishi Wetu,Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amewataka Watanzania kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta ya hifadhi ya mazingira ili kujiongezea kipato na kujiinua kiuchumi.
Dkt. Kijaji amesema hayo leo Ahamisi Agosti 8, 2024 wakati alipotembelea Banda la Maonesho la Ofisi hiyo katika kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Duniani (Nanenane) yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma.
Waziri Kijaji amesema katika kuhakikisha sekta ya hifadhi ya mazingira inaendelea kuwanufaisha Watanzania wengi zaidi, Ofisi hiyo imeanisha vipaumbele sita vya kimkakati na kuvitangaza kupitia elimu ya maonesho na hivyo kuwataka wananchi kuchangamkia fursa hizo.
Amebainisha vipaumbele mojawapo ni biashara ya kaboni ambayo kwa sasa imeanza kushika kasi hapa nchini ambapo Serikali tayari imeandaa kanuni na miongozo mbalimbali inayolenga kuwanufaisha Watanzania.
“Hii ni biashara ambayo fursa yake ipo zaidi kupitia misitu pamoja na taka ngumu ambayo vyote kwa pamoja tafsiri yake ni hifadhi ya mazingira….. Tunawahimiza Watanzania kuchangamkia fursa hii kwani kwa sasa milango wazi kwa jamii kunufaisha” amesema Dkt. Kijaji.
Aidha Dkt. Kijaji ametaja kipaumbele kingine ni pamoja na masuala ya uchumi wa buluu, ambapo Ofisi hiyo imepanga kutangaza fursa zilizopo katika rasilimali maji ikiwemo bahari, maziwa na mito katika namna zinavyoweza kuwanufaisha Watanzania kwa kuwainua kiuchumi.
Waziri Kijaji ametaja kipaumbele kingine ni pamoja na fursa za mfumo wa uchakataji wa taka ngumu kupitia teknolojia ya urejelezaji ambapo sanjari na kutahifadhi mazingira, mfumo huo pia utaweza kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Akifafanua zaidi Waziri Kijaji ameeleza kuwa kutokana na jamii kupata mwamko kuhusu fursa za urejelezaji wa taka ngumu, Ofisi hiyo imepanga kujenga viwanda vya kuchakata taka katika majiji mbalimbali nchini ambapo kwa kuanzia kituo cha aina hiyo kimepangwa kujengwa katika Jiji la Dodoma.
“Tunataka katika kipindi cha miaka miwili ijayo Ofisi ya Makamu wa Rais tuwe na Muungano Imara na Miji iliyo safi na salama kwa mazingira yetu na jamii yetu kwa ujumla na kwa kufanya hivi kila Mtanzania atafahamu kwa mapana manufaa na umuhimu wa Ofisi hii” amesema Dkt. Kijaji.
Ameongeza kuwa pamoja na kuweka mkazo hifadhi ya mazingira, Ofisi hiyo pia imekusudia kuongeza wigo wa programu ya elimu kwa umma kuhusu masuala ya Muungano kwa kuhakikisha jamii inafahamu chimbuko na misingi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kwa mujibu wa Waziri Kijaji amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa sasa una zaidi ya miaka 60 ambapo kwa mujibu wa takwimu zilizopo zinaonesha kuwa idadi kubwa ya Watanzania ni vijana ambapo wanahitaji elimu ya kutosha kuweza kuelewa misingi ya kuasisiwa kwa Muungano huo.
“Kundi kubwa la Watanzania walizaliwa baada ya Muungano, hivyo ni wachache wenye uelewa kuhusu Muungano…Tumepanga kuhakikisha kuwa elimu ya Muungano inaendelea kutolewa kwa Watanzania ili waweze kufahamu nini chimbuko la Muungano huu uliaosisiwa na Viongozi wetu” amesema Dkt. Kijaji.
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) imeungana na Taasisi na Idara mbalimbali za Serikali kushiriki maonesho ya maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Duniani (Nanenane) yenye kauli mbiu isemayo “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi”
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili katika Banda la Ofisi hiyo katika Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Duniani (Nanenane) yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma leo Alhamisi Agosti 8, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Ofisi hiyo, Bi. Sarah Kibonde muda mfupi baada ya kuwasili katika Banda la Ofisi hiyo katika Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Duniani (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma leo Alhamisi Agosti 8, 2024
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na Waandishi wa Habari kutoka Kampuni ya Ndalini Media wakati alipotembelea Banda la Ofisi hiyo katika Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Duniani (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma leo Alhamisi Agosti 8, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na mwandishi wa Habari kutoka Kampuni ya Ndalini Media wakati alipotembelea Banda la Ofisi hiyo katika Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Duniani (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma leo Alhamisi Agosti 8, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakati alipotembelea Banda la Ofisi hiyo katika Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Duniani (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma leo Alhamisi Agosti 8, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea Banda la Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) katika Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Duniani (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma leo Alhamisi Agosti 8, 2024. Wa kwanza kulia ni Meneja wa NEMC Kanda ya Kati Dodoma Dkt. Caren Kahambwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) akipokea nyaraka mbalimbali zilizoandaliwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutoka kwa Meneja wa NEMC Kanda ya Kati Dodoma Dkt. Caren Kahambwa katika Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Duniani (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma leo Alhamisi Agosti 8, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akipata maelezo kutoka kwa Katibu wa Kikundi cha NOPADEO WOMEN, Bi. Eneles Sohoma kuhusu mafanikio ya Mradi wa Urejeshaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Baianoai Tanzania (SLR) unaotekelezwa katika kijiji cha Matebete Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya wakati alipotembelea Banda la Mradi huo wakati alipotembelea Banda la Mradi huo katika Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Duniani (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma leo Alhamisi Agosti 8, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akipokea zawadi ya maziwa kutoka kwa wanakikundi wa NOPADEO WOMEN kutoka Kijiji cha Matebete Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya wanaotekeleza Mradi wa Urejeshaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Baianoai Tanzania (SLR) wakati alipotembelea Banda la Mradi huo katika Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Duniani (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma leo Alhamisi Agosti 8, 2024. Anayekabidhi zawadi hiyo ni Mwanakikundi wa NAPODEO WOMEN Bi. Juliana Israeli.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akipokea nyaraka mbalimbali zilizoandaliwa na Ofisi hiyo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Bi. Sarah Kibonde wakati alipotembelea Banda la Ofisi hiyo katika katika Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Duniani (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma leo Alhamisi Agosti 8, 2024.
(NA MPIGAPICHA WETU)
No comments:
Post a Comment