DKT. TULIA AMTEMBELEA MTOTO ALIOFANYIWA UPASUAJI KUONDOLEWA UVIMBE SHINGONI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, August 5, 2024

DKT. TULIA AMTEMBELEA MTOTO ALIOFANYIWA UPASUAJI KUONDOLEWA UVIMBE SHINGONI


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson leo amtembelea na kumjulia hali mtoto Debora Saimon aliofanyiwa upasuaji wa kuondolewa uvimbe sehemu ya shingoni katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.


Akizungumza mara baada ya kumtembelea na kumjulia hali mtoto Debora, Dkt. Tulia amepongeza watoa huduma wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa jitihada walizozichukua kwa muda mfupi katika kutoa huduma nzuri, vilevile ameushukuru Uongozi wa Hospitali kwa ushirikiano mzuri anaoendelea kupata pindi kunapojitokeza changaoto za msaada wa kimatibabu kwa wananchi wa Mbeya.


Nae Dkt. Godlove Mbwanji Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, amemshukuru Mheshimiwa Spika Tulia Ackson kwa kuitembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya mara kwa mara na kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa katika kuwahudumia wananchi wa Nyanda za Juu Kusini na kueleza kuwa uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya awamu ya 6 chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluh Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, umeiwezesha hospitali kutoa huduma za uhakika na za kibingwa na kupunguza rufaa za kupelekwa wagonjwa hospitali ta Taifa jijini Dar es Salaam

Hapo awali Mama mlezi wa Deborah Alen Mwakisombole alifika kwenye moja ya mikutano ya hadhara ya Mhe. Dkt. Tulia Ackson katika jimbo lake la Mbeya Mjini na kuomba kusaidiwa matibabu na ya mwanaye huo.

No comments:

Post a Comment