KIKAO KAZI CHA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA NA OFISI YA RAIS-UTUMISHI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, August 22, 2024

KIKAO KAZI CHA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA NA OFISI YA RAIS-UTUMISHI

Baadhi ya Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Watendaji wa PCCB wakifuatilia jedwali lenye ufafanuzi wa maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa katika ukumbi mdogo wa Bunge jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent L. Kyombo akizungumza na Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Watendaji wa PCCB (hawapo pichani), wakati wa kikao cha kupokea ufafanuzi wa maoni kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akifafanua jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria cha kupokea ufafanuzi wa maoni kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa katika ukumbi mdogo wa Bunge jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakifuatilia maelezo ya ufafanuzi wa maoni ya kamati hiyo kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Chalamila wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria cha kupokea ufafanuzi wa maoni kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa katika ukumbi mdogo wa Bunge jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akizungumza na wageni kutoka Taasisi ya Uongozi waliofika ofisini kwake kupata maelekezo ya namna ya kufanya Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Taasisi hiyo, Mtumba Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment