MHANDISI MSHAURI TARURA AELEZEA UMUHIMU WA MADARAJA NA BARABARA ZA MAWE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, August 5, 2024

MHANDISI MSHAURI TARURA AELEZEA UMUHIMU WA MADARAJA NA BARABARA ZA MAWE


Na Mwandishi Wetu , Dodoma


Mhandisi Mshauri kutoka Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ambaye pia ni Mratibu wa madaraja na barabara za mawe, Mhandisi Pharles Ngeleja ameeleza umuhimu wa matumizi ya teknolojia ya madaraja na barabara za mawe katika ujenzi wa barabara.

Amesema hayo katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Amesema lengo ni kufanya kazi nzuri ya ujenzi wa barabara na madaraja kwa kutumia teknolojia ya mawe ili kupunguza gharama na kupata barabara imara ili ziweze kuwasaidia wananchi kuondokana na changamoto mbalimbali za usafiri. 

“Jambo kubwa tunalolifanya TARURA ni kufanya ujenzi pamoja na ukarabati wa barabara nchini na sasa tunajenga barabara na madaraja kwa kutumia teknolojia ya mawe ili kuwawezesha wakulima kusafirisha mazao yao kutoka vijijini kwenda mjini na kusafiri kwa urahisi kuzifikia huduma za kijamii.

Ameongeza kusema kuwa wamejenga madaraja 250 ya mawe nchi nzima na mkoa wa Kigoma ndio unaoongoza pia mikoa ya Mwanza na Morogoro ni baadhi ya mikoa iliyonufaika na teknolojia hiyo. 


Naye, Bi. Catherine Sungura Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano (TARURA) ameongeza kusema kuwa TARURA wamejenga madaraja mengi hasa vijijini na hivi juzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua daraja ambalo limetengenezwa na TARURA lengo likiwa kuwasaidia wananchi kufanya shughuli zao kwa urahisi ikiwemo kwenda kufuata huduma za kijamii.

No comments:

Post a Comment