MTI WA MBUYU KATIKA KITUO CHA MBUYUNI HAUTAATHIRIWA NA UJENZI WA MABASI YAENDAYO HARAKA (BRT 4), JIJINI DAR ES SALAAM - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, August 1, 2024

MTI WA MBUYU KATIKA KITUO CHA MBUYUNI HAUTAATHIRIWA NA UJENZI WA MABASI YAENDAYO HARAKA (BRT 4), JIJINI DAR ES SALAAM


Serikali kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS) inaendelea na ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam Awamu ya Nne (BRT 4) kuanzia Daraja la Kijazi (Sam Nujoma) - Mwenge - Maktaba ya Taifa (Posta) yenye urefu wa kilometa 13.5 huku moja ya lengo likiwa ni kuufungua Mkoa wa Dar es Salaam kwa Miundonbinu ya uhakika ili kutatua kero za foleni za magari.

Kwa sasa Mkandarasi anayetekeleza mradi huo anafanya maandalizi ya usafishaji (Site clearance and top soil removal) katika eneo la katikati ya barabara ambapo njia ya BRT itajengwa bila kuathiri uwepo wa Mbuyu huo.

Kazi hiyo ya usafishaji kwa vyovyote vile itafanyika bila kuathiri mti wa Mbuyu uliopo karibu na kituo cha Mbuyuni, wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam. 

Hayo yamesemwa na Msaidizi wa Meneja Mradi wa BRT 4 Mhandisi Leocard Sikambale akiwa katika eneo hilo la mradi. 

"Mkandarasi anaendelea na maandalizi ya kufanya (clearance) hapo katikati ili kujenga njia na kituo cha Mabasi ya Mwendokasi (BRT), na kazi hiyo itafanyika bila kuathiri mbuyu huo" alisisitiza Mhandisi Sikambale

No comments:

Post a Comment