Rais Dkt. Samia aiambia TFRA ichape kazi kilimo kitatuinua - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, August 9, 2024

Rais Dkt. Samia aiambia TFRA ichape kazi kilimo kitatuinua

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi TFRA, Dkt. Anthony Diallo alipotembelea banda la Mamlaka wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mkulima- nanenane Nzuguni Jijini Dodoma tarehe 8 Agosti, 2024
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea taarifa ya utendaji kutoka kwa Mwenyekiti wa bodi ya TFRA, Dkt. Anthony Diallo alipotembelea banda la Mamlaka wakati wa kilele cha maadhimisho ya sikukuu za wakulima - nanenane zilizofanyika Kimataifa katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma tarehe 8 Agosti, 2024


Na Mwandishi Wetu Dodoma 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua na kugawa Hati ya Hakimiliki Ardhi ya kimila pamoja na kitambulisho janja (farmer smart card) kwa wakulima waliokidhi vigezo.

Akiwa mkulima namba moja Mhe. Rais amekabidhiwa kadi hiyo pamoja na wakulima wengine Saba kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Kitambulisho hicho kimeunganishwa na mifumo mbalimbali kama vile NIDA, Ardhi, kadi ya Jamii, Benki na pembejeo za ruzuku kitakachomwezesha mkulima kupata huduma mbalimbali za kifedha kama vile kutoa na kuweka fedha benki, kupokea malipo ya mauzo ya mazao yake, huduma za bima zikiwemo bima za afya, bima za pembejeo kwa atakayehitaji na kukidhi vigezo.

Uzinduzi huo umefanyika tarehe 8 Agosti, 2024 wakati wa kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane yaliyofanyika Kimataifa katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma na kuipongeza TFRA kwa kazi nzuri na kuitaka iendelee kuwahudumia wakulima.

Akikagua vipando vilivyoandaliwa na wilaya na halmashauri za mikoa ya Kanda ya Kati yaani Singida Dodoma na Manyara, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameeleza kuwa vipando hivyo vimehudumiwa kwa mbolea zinazoingizwa kutoka nje ya nchi na zile zinazozozalishwa nchini ili kuwasaidia wakulima kuondokana na dhana kwamba mbolea zinazozalishwa nchini hazifanyi vizuri isipokuwa zinazoingizwa kutoka nje ya nchi.

Amesema, kupitia vipando hivyo, wakulima wamejifunza kwa macho na kuona nana mazao yaliyolimwa na kuhudumiwa kwa mbolea zinazozalishwa nchini yamestawi vizuri tofauti na Imani zao.

Akizungumza kwa niaba ya wakulima wote nchini ndani ya banda la Mamlaka, Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA, Dkt. Anthony Diallo ametoa shukrani kwa maamuzi ya kutekeleza mpango wa mbolea za ruzuku kuanzia msimu wa kilimo wa 2022/2023 na 2023/2024, na kwa kukubali kuendelea kutoa ruzuku hiyo hadi msimu wa kilimo wa 2025/2026.

Amesema, mpango huo umekuwa na matokeo chanya kwa wakulima na sekta ya kilimo kwa ujumla.

Akieleza tija iliyotokana na utekelezaji wa mpango huo, Dkt. Diallo amesema, tija ya uzalishaji imeongezeka kutoka tani 17,148,290 mwaka 2021/2022 hadi kufikia tani 20,402,014 mwaka 2022/2023.

Aidha, matumizi ya mbolea nchini yameongezeka kutoka tani 363,000 katika msimu wa kilimo wa 2021/2022 hadi kufikia tani 840,000 katika msimu wa kilimo wa 2023/2024.

Tunatarajia matumizi ya mbolea kuongezeka zaidi hadi kufikia tani 1,000,000 ifikapo mwishoni mwa msimu wa 2024/2025.Hii inazidi malengo ya Abuja yaliyowekwa na nchi za Afrika mwaka 2006, ambapo walikubaliana kuwa matumizi ya mbolea yafikie kilo 50 kwa hekta moja ifikapo mwaka 2025.

"Mheshimiwa Rais, mpango huu pia umetuwezesha kuwatambua wakulima na maeneo yao ya uzalishaji", Dkt. Diallo amesema.

Tunakupongeza kwa juhudi hizi na tunatumaini kuwa mafanikio haya yataendelea kukua na kuleta mabadiliko makubwa zaidi katika sekta ya kilimo na maisha ya wakulima nchini.

Kwa Upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA amewataka wakulima ambao bado hawajasajiliwa au kuhakiki taarifa zao kufanya hivyo sasa ili wasipitwe na fursa hizo adhimu wenye mfumo wa mbolea za ruzuku.

No comments:

Post a Comment