MAONESHO YA BIASHARA YA TANZANITE MANYARA TRADE FAIR 2024 KUFANYIKA OCTOBA 20-30 MWAKA HUU. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, August 9, 2024

MAONESHO YA BIASHARA YA TANZANITE MANYARA TRADE FAIR 2024 KUFANYIKA OCTOBA 20-30 MWAKA HUU.


Na Mwandishi Wetu ,Manyara.


Maonesho ya tatu ya Biashara,Viwanda na Kilimo ya Tanzanite Manyara Trade Fair 2024 yanatarajiwa kufanyika Octoba 20 hadi 30 mwaka huu katika viwanja vya Tanzanite Kwaraa Stedium mjini Babati mkoani Manyara huku wafanyabiashara zaidi ya 500 wataonesha bidhaa mbali mbali na teknolojia mbali mbali za kuongeza thamani ya Mazao ya Nafaka.


Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga akizungumza na Wanahabari ofisini kwake amesema kuwa maonesho hayo yameandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara pamoja na SIDO Manyara ambapo wajasiriamali watapata fursa ya kutangaza biashara zao na kupata fursa za masoko.

Sendiga amewakaribisha Wajasiriamali kote nchini kushiriki maonesho hayo muhimu na kujionea bidhaa zinazozalishwa Manyara pamoja na fursa mbali mbali zilizopo.

Aidha Sendiga amesema kuwa zaidi ya watu 40,000 watashiriki kwenye maonesho hayo kutoka ndani na nje ya nchi ya Tanzania.


Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Mkoa wa Manyara (TCCIA) Musa Msuya amewataka Wafanyabiashara kutoka sehemu mbali mbali nchini kuchangamkia fursa za maonesho hayo kwa kushiriki na kupata masoko ya uhakika.


Kwa Upande Wake Afisa Masoko Kampuni ya Mati Super Brands Limited Gwandumi Mpoma amesema kuwa kampuni hiyo imeamua kudhamini maonesho hayo ili kuunga mkono jamii ikiwemo wajasiriamali wadogo na wakati kupata fursa ya kujitangaza kupitia maonesho hayo.

Kauli mbiu ya maonesho hayo ni "Manyara kwa ustawi wa biashara na uwekezaji "

No comments:

Post a Comment